Kutajwa kwa Mbowe: Kisa ni Billicanas inayomilikiwa na Mbowe Hotels

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
22,227
49,627
Imefahamika kuwa Mbowe alitajwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa vile ni mmiliki wa Mbowe Hotels inayoendesha ukumbi maarufu wa Billicanas.

Inasemekana ukumbi wa Billicanas ambao huwa unatumiwa na wanamziki wengi mastar na wafanyabiashara wakubwa kilikuwa kama kituo kinachotumiwa na wauza unga kukutana.

Wadadisi wa mambo wanasema Mbowe amehusishwa kwa sababu za kisiasa tu, mhusika ambaye angetakiwa kuitwa ni meneja wa hotel au meneja wa ukumbi na siyo Mbowe binafsi ambaye hata baadhi ya watumishi wa hotel hiyo waliochini ya mameneja hawajui na wageni wanaoingia pale hawajui.

Nawasilisha.
Makonda anazidi kuumbuka

652b9d7e2407ac1e7584c7f2ca8691ac.jpg

fe687bd2e091811772a5a9d429230680.jpg

MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Viongozi wa Dini, Askofu Wiliam Mwamalanga, amesema amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja Freeman Mbowe kuwa miongoni mwa watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Askofu Mwamalanga alisema kamati yao ilitilia shaka Bilicanas iliyokuwa inamilikiwa na Kampuni ya Mbowe Hotels, kwamba ni moja ya maeneo yanayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kufanya biashara zao, lakini si mwanasiasa huyo.

Alisema ukumbi huo wa starehe kuhusishwa na biashara hiyo, haikumaanisha kwamba mmiliki wake ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anahusika.

“Sisi tulisema klabu ya Bilinacas inajihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya kwa sababu walikuwa wanaingia watu mbalimbali ambao walikuwa wakiendesha shughuli hizo, lakini hatukumtaja mmiliki wake Mbowe ndiye anayejihusisha na dawa hizo,” alisema Askofu Mwamalanga.

Alisema kamati hiyo itashirikiana na Serikali ili kuhakikisha biashara ya dawa za kulevya inatokomezwa na wahusika wote wanafikishwa kwenye mikono ya sheria.

Kamati hiyo pia imempongeza Rais Dk. John Magufuli kumteua Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya mwenye taaluma ya kusimamia suala hilo, jambo ambalo limesaidia kutotajwa watuhumiwa hadharani badala yake wahusika waweze kuchukuliwa hatua.

Chanzo: Mtanzania
 
Imefahamika kuwa Mbowe alitajwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa vile ni mmiliki wa Mbowe Hotels inayoendesha ukumbi maarufu wa Billicanas.

Inasemekana ukumbi wa Billicanas ambao huwa unatumiwa na wamziki wengi mastar na wafanyabiashara wakubwa kilikuwa kama kituo kinachotumiwa na wauza unga kukutana.

Wadadisi wa mambo wanasema Mbowe amehusishwa kwa sababu za kisiasa tu, muhusika mkuu angekuwa meneja wa hotel au meneja wa ukumbi na siyo Mbowe binafsi ambaye hata baadhi ya watumishi wa hotel hiyo waliochini ya mameneja hawajui.

Nawasilisha.

TISS wako wapi na wanafanya kazi gani? Kazi ya TISS kwani ni kusimamia kura ya turufu kwenye uchaguzi na kufanyizia wapinzani?

Meneja wa hotel au ukumbi ndio huwa wanashirki mambo yote yafanywayo na wateja wao?

Hawa mameneja huwa wanalazimika kuhakikisha wateja wote wanoingia mle ni marafiki au ni watu wanaofahamiana nao tu?

HIvi kweli waache kazi ya kumeneji waanze kuchunguza ni shughuli gani wateja wao wanafanya n ahata kama ni wanamziki wana maisha gani ya pili?

Acheni utani bwana!
 
Kweli Kabisa, Na kwasababu hilo jengo walikuwa wanamiliki pamoja na NHC basi ata yule kibosile wa pale alitakiwa kutajwa kwa hiyo maneno. Hata hivyo lazima wangeangukia pua mahakamani manake FAM angesema wamwonyeshe hiyo Bilinkanasi ilipo
 
Ile ni shughuli ya chama! Eti shughuli ya kitaifa tunaita akina madabida waanze kutoa historia ya chama na bla bla nyiiiingi!
Kubafu kabisa
Hivi ile scandal yake na mkewe kuuzia Watz ARV feki iliishia wapi mkuu?
 
waliitwa wamiliki wa casino nyingi tu

mbowe angeenda na kusafisha hali ya hewa

kujifanya kugoma, kuna watu wanazua maswali mtaani...
Uitwaji wa wale upo tofauti na huu wa Mbowe!!

Kwa mfano, Makonda alitamka wazi kwamba Mmiliki wa Slipway (kama sikosei) anamiliki private dock inayotumika kupaki boti zake pale kwa wajili ya wateja!!

Lakini bandari hiyo binafsi pia anaitumia kama bandari ya kushusha mihadarati!!!

Kwahiyo katika mazinigira kama hayo moja kwa moja inaonesha ni shughuli ya Slipway wenyewe na sio wateja!!

Hata hivyo, nasikia baada ya kuhojiwa imeonekana hamna kitu kama hicho... ujinga ule ule tuliokuwa tunausema!!!
 
Imefahamika kuwa Mbowe alitajwa kuhusika na madawa ya kulevya kwa vile ni mmiliki wa Mbowe Hotels inayoendesha ukumbi maarufu wa Billicanas.

Inasemekana ukumbi wa Billicanas ambao huwa unatumiwa na wanamziki wengi mastar na wafanyabiashara wakubwa kilikuwa kama kituo kinachotumiwa na wauza unga kukutana.

Wadadisi wa mambo wanasema Mbowe amehusishwa kwa sababu za kisiasa tu, mhusika ambaye angekiwa kuitwa ni meneja wa hotel au meneja wa ukumbi na siyo Mbowe binafsi ambaye hata baadhi ya watumishi wa hotel hiyo waliochini ya mameneja hawajui na wageni wanaoingia pale hawajui.

Nawasilisha.
Political sentiment. Kama Bilicanas ilikuwa chini ya Mbowe, basi anapaswa kufafanua ilikuwaje ikageuzwa kitovu cha wauza unga. Serikali haimtambui meneja kama mmiliki.
 
Political sentiment. Kama Bilicanas ilikuwa chini ya Mbowe, basi anapaswa kufafanua ilikuwaje ikageuzwa kitovu cha wauza unga. Serikali haimtambui meneja kama mmiliki.
Kama serikali inatambua kuwa Bilicanas iligeuzwa kitovu cha wauza unga ilishindwaje kuwakamata hhao wauza unga halafu leo ilete majungu?
 
Back
Top Bottom