Kutaanzishwa mamlaka ya kulinda msingi wa viwanda na rasilimali za nchi

Kutaanzishwa mamlaka ya kulinda msingi wa viwanda na rasilimali za nchi

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
4,124
Reaction score
6,141
Nikiwa Rais wa Tanzania kutaanzishwa hii taasisi ya kupigania maslai ya kiuchumi, rasilimali Tanzania tofauti na usalama wa Taifa ambao utaendelea na jukumu lake la kulinda viongozi

Hii taasisi itakuwa na kazi zifuatazo;-
  1. Kutafuta waekezaji wa smelter na refining za aina zote na kuzilinda kwa gharama yote kama msingi wa viwanda.
  2. Kuvutia waekezaji wa viwanda vya secondary mfano viwanda vya magari, simu, nguo, viatu, pharmaceutical, na kuhakikisha gharama za uzalishaji zinakuwa chini sana.
  3. Kuhakikisha umeme unazalishawa mwingi sana ili uweze kupunguza gharama za viwanda Tanzania.
  4. Kupigania masoko ya nje ya bidhaa zinazozalishwa Tanzania.
  5. Kuhakikisha gharama za uzalishaji zinakuwa chini sana hapa Tanzania
  6. Kuhakikisha mikataba ya madini na rasilimali nyingine zinainufaisha nchi.
  7. Kuhakikisha rasilimali za nchi hazinufaishi watu wachache na kuzuia ufisadi kwenye rasilimali za nchi.
  8. Kuitetea nchi kama zikitokea kesi za mikataba na wawekezaji ndani na nje ya nchi.

Uongozi wa hii taasisi
  • Kiongozi atakuwa anachaguliwa na Rais bali hataweza kumuondoa baada ya miaka 3 kupita
  • Kama akiingia Rais mwingine anaweza muondoa au akamuacha
 
Una mawazo mazuri ila nadhani priority yako iwe kupunguza deni la nchi kwanza.
Lazima kuwe na taasisi imara ili deni lipunguzwe moja ya mambo niliyoyapropose ni kufanya auditing kwenye deni la taifa nimeongelea kwenye huu uzi
 
Lazima kuwe na taasisi imara ili deni lipunguzwe moja ya mambo niliyoyapropose ni kufanya auditing kwenye deni la taifa nimeongelea kwenye huu uzi

Ok Mkuu nimekupata.
 
Back
Top Bottom