Kususa kwa wabunge wa upinzani hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,611
Asubuhi ya siku ya uchaguzi mwaka jana nilikwenda kumpigia kura rais, diwani na mbunge. Kura ni siri, siwezi kusema nilimpigia nani.

Kitu ambacho sikutegemea kukiona ni kumuona mbunge wa jimbo langu akiwa ni mmojawapo wa wabunge ambao badala ya kushughulika na shida zetu wananchi wa jimbo lake, akiwa mstari wa mbele katika kufanya kila liwezekanalo ili Dr Tulia aweze kutolewa kwenye nafasi ya naibu spika.

Wakati wa kampeni mpaka kupiga kura hakuna mpiga kura hata mmoja ambaye angeweza kwa akili zinazofanya kazi kabisa, kudhani kwamba mbunge aliyeamka mapema alfajiri ili ampigie kura angeweza kusahau sababu ya yeye kuwa mbunge na kuwa mwanaharakati wa kumuondoa naibu spika.

Mbunge hakutumwa bungeni ahangaishane na cheo cha naibu spika, ametumwa atetee maslahi ya mwananchi wa kawaida.

Bajeti kuu imeshapita, serikali inakwenda kutekeleza yote ambayo yamewakilisha na mawaziri. Uhalali wa mgomo wa wabunge wa upinzani upo katika serikali kushindwa kutimiza yale yaliyoainishwa kwenye bajeti, vinginevyo kama serikali itasimamia utekelezaji wa bajeti, heshima ya wabunge wote waliogoma itakuwa imeshuka kwa wananchi walioamka alfajiri na kwenda kuwapigia kura.

Siasa zina muda wake, tena siku zote unapaswa kuheshimiwa. Na utafutaji wa maendeleo na wenyewe una muda wake, tena siku zote ni mwingi kuliko ule unaotumika kwenye siasa, na siku zote unapaswa kuheshimiwa.

Mungu ibariki Tanzania, uzibariki nia na malengo aliyonayo kila mtanzania ili taifa liweze kustawi.
 
Back
Top Bottom