Mi naomba ushauri,,,,
Nina matatizo na tigo, wanakula hela zangu ile mbaya, ilifikia hatua kuwa nikiuliza salio najibiwa in terms of negative, yaani na daiwa, wakati sijawahi kuchukua mkopo, vile vile, kifurushi cha internt sio 24 hrs kama wanavodai, nikiunga saa 4 usiku natumiwa message kuwa mpaka saa 4 usiku ya siku ya pili kifurushi ndo kitaisha, kumbe ikifika saa 6 usiku ule nloinganisha kifurushi hakifanyi kazi tena, na ukitaka kujiunga na chengine wanakwambia bado upo kwenye kifurushi, kuna siku nyengine nlijiunga na sms zao, hazikufika mia zikagoma kwenda, nkajaribu kuuliza salio nikajibiwa ninazo kiasi fulani za message lakini bado zikawa haziendi, nikavumilie kidogo, kisha nkauliza tena salio nkashangazwa kwa jibu nlopata, message ni zero zeroooo!! Ukiingia facebook na kuitizama page yao utakuta lawama kibao na hawazishuhulikii, customer care utakaa 2 hours umewekwa hold kwenye simu unaambiwa mhudumu yuko bize, PAGE ya FB hawakujibu pia,,,, yani wizi kwenda mbele! Hii TCRA ina umuhimu gani?