DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Mkuu wa Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Kissa Kasongwa, ameagiza mkandarasi wa mradi wa maji wa Ipelele kufika ofisini kwake haraka ili kutoa maelezo ya kina juu ya kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo, licha ya serikali kutoa fedha zote zinazohitajika.
Akizungumza baada ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Ipelele, DC Kissa amesema kuwa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 358.2, ulipaswa kuwa umekamilika kwa sasa, lakini badala yake umeendelea kuongezewa muda bila mafanikio yoyote makubwa, huku wananchi wakikabiliwa na adha kubwa ya maji safi na salama.
“Uje na mkandarasi ofisini kwangu Jumatano. Nataka anieleze kwanini kila siku anaongezewa muda. Kama hawezi, tuchukue hatua nyingine. Wananchi hawataki visingizio, wanahitaji huduma ya maji,” amesema kwa msisitizo DC Kissa.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ipelele akiwemo Mwipelel Mbogela na Juaji Ngailo, walisema wamechoshwa na ahadi zisizoisha huku wakikumbwa na shida ya maji kwa muda mrefu licha ya mradi huo kupewa kipaumbele.
“Tunaambiwa fedha zipo, lakini hatuoni maji. Tunataka tujue shida ni nini hasa. Huu ni mwaka wa tatu tangu mradi uanze, maji bado,” alisema Ngailo.
Akitoa ufafanuzi, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Makete, Mhandisi Innocent Lyamuya, amesema mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya MP Groups, umefikia asilimia 45 ya utekelezaji na kwamba mkandarasi ameomba kuongezewa muda hadi mwezi Agosti mwaka huu.
“Ni kweli mradi unachelewa. Lakini sisi kama RUWASA tumeendelea kumsimamia. Serikali haitadaiwa chochote katika huu mradi, hivyo tunamtaka amalize kama alivyoahidi,” amesema Lyamuya.
Kwa mujibu wa DC Kasongwa, serikali ya wilaya haitasita kuchukua hatua za kisheria au kuvunja mkataba endapo mkandarasi ataendelea kuchelewesha mradi huo ambao ni wa matumaini kwa wananchi wa Ipelele na vijiji vya jirani.

Chanzo: Jambo Tv