ubuntuX
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 1,977
- 2,200
Wahitimu wa miaka miwili sasa wamekaa mtaani bila kutumikia jamii na kufanya uzalishaji unaotakiwa kwa maendeleo ya nchi.
Hii ni kupoteza nguvu kazi ya taifa, hawa vijana wangeiishia form four tu na wangekuwa wanafanya shughuli nyingine za uzalishaji kama kilimo, biashara na kufanya kazi ngumu zisizohitaji akili.
Nini mantiki ya kutumia gharama kubwa kusomesha vijana pasipo nao kutumika baada ya kuhitimu masomo yao? Serikali mnatakiwa mjitizame upya, hakuna maana ya kusoma sasa bora mkaachana na mpango wa kugharamia elimu ya juu ambayo kwa sasa haina tija kwa taifa.
Badala yake mjikite na elimu bure inayoishia form four vijana wakimaliza wakalime tu.