Kushangaa bata akiogelea kwenye maji machafu ni ushamba

Kushangaa bata akiogelea kwenye maji machafu ni ushamba

Obby

Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
5
Reaction score
2
Kuna siku nakumbuka niliwahi kukaa na vijana wa umri wangu tukawa tunajadili kitu flani hivi,kati kati ya mada japo sikumbuki vizuri mada ilikua inasemaje.Nikawaambia wenzangu kuwa katika mabunge ya wenzetu,mfano mzuri Bunge la Russia ni kwamba Mgombea wakiti cha Spika anatakiwa awee na cheti chochote cha mafunzo ya mapigano(kwa kimombo Martial Art Certified Certificate).
Wakanibishia kweli,but mimi sikutaka mabishano nao kwakua hawakunielewa ni nini nilikua namaanisha,sasa yamejitokeza wiki hii nkawafata na kuwakumbushia,japo sio wote walielewa,kwa bahati nzuri akatokea mmoja kati yao akaniambia kuwa "Obby,sasa nimekuelewa ulichokua unakisema,kwa style ile ya Bunge la sasa ni kweli anahitajika Spika mwenye mkanda mweusi ili kuamua ugomvi".
Sioni mantiki ya polisi kuingia Bungeni na kumtoa Mbunge anayewakilisha wananchi,yaani ni sawa na kumtoa rais ikulu,then tunahoji ukimtoa yeye ikulu akalale wapi(japokuwa ana nyumba nyingi) sasa kazi za kuwawakilisha wananchi atazifanyia wapi.
Hao wanaojifanya kushangaa vurugu bungeni waende Russia,India,China,Thailand wakajionee yanayotokea ndipo wataelewa ninachokisema.
pale wamekutana watu tofauti wenye mawazo tofauti,sera,tabia nazo tofauti.Sasa kwa swala la kutukana,kugombana,kutokuelewana ni jambo la kawaida kama jogoo kuwika asubuhi.
 
Back
Top Bottom