Kuscroll video mitandaoni huaribu maisha kwa kiasi kikubwa

joseph_mbeya

JF-Expert Member
Nov 20, 2023
252
586
Ukiwa ni mmoja wa watumiaji nguli wa mitandao yenye platform ya shorts videos kama
  1. Instagram
  2. Twitter (x)
  3. YouTube (shorts)
  4. tik tok
  5. Snapchat.

na kadhalika najua umewahi pitia hali fulani hivi unajikuta umescroll video muda mrefu mpaka unaangalia saa unabaki unashangaa mbona muda umeenda fasta hivi basi hivo ndivi unajiharibia maisha na hivo ndivo unajiongezea uwezekano wa kupata misongo ya mawazo
Hizo ni baadhi ya athari za kuscroll videos mitandaoni kwa muda mrefu 👇
1. Upotezaji wa Muda: Kuscroll video kwa muda mrefu kunaweza kusababisha upotezaji wa muda unaoweza kutumika kwa shughuli nyingine muhimu, kama kazi au masomo.

2. Kupungua Kwa Umakini: Matumizi ya muda mwingi mitandaoni yanaweza kusababisha kupungua kwa umakini, na hivyo kushindwa kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

3. Athari za Kijamii: Kusalia kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kunaweza kusababisha kutengwa kijamii na kupungua kwa mwingiliano wa moja kwa moja na watu wa karibu.

4. Mabadiliko ya Tabia: Video nyingi mitandaoni zinaweza kuathiri tabia za watu, ikiwa ni pamoja na mtazamo wao kuhusu mwili, mahusiano, na maadili, ambayo yanaweza kuwa na athari za kudumu.

5. Udhibiti wa Hisia: Baadhi ya video zinaweza kuathiri hisia za watu kwa kutoa taarifa au maudhui yenye mzozo, na hivyo kuathiri hali yao ya kihemko.

6. Kupoteza Fursa za Kujifunza: Muda uliotumika kuscroll video unaweza kuzuia fursa za kujifunza na kukua, kwani unaweza kutoweka muda ambao ungeweza kutumika kwa shughuli za kujenga ujuzi au elimu.

Kwa kuzingatia haya, ni muhimu kuwa na udhibiti mzuri wa muda na kuchagua kwa makini aina ya maudhui unayotumia muda wako kuiona mtandaoni.

MI pia nilikuwa muanga wa hilo jambo lakini nilijitahidi sana kuacha haikuwa rahisi sana kuacha lakini mpaka sasa natumia mitandaoni miwili tu ya kijamii ambayo ni jamiiforum na Whatsapp, telegram(natumia sababu za kikazi) na sidhani kama nahitaji mitandaoni mengine zaidi sababu kama ni habari napitia chrome nacheki tovuti za habari then naacha nazo
Screenshot_20231226-131459.png
 
Na pia sidhani kama kuna faida za kutumia hiyo mitandao kwa kijana ambae bado unajitafuta
 
Kila mtu apambane na hali yake, kila mtu akiwa makini nani atakuwa kibarua wa mwenzake.
 
Mtoa mada na watu wengi wanashindwa kutofautisha MAKING and SPENDING, si kilamuda ni wa Making kuna muda wa SPENDING na kuperuzi ni moja ya njia ya SPENDING baada ya kufanya making.

Kisema umefuta Social network zote sawa na kusema wewe kwenye Marshall yako ni making tu bila kufanya spending yawning kwa luggage ragusa ni unatafuta Maisha tu na si kuishi
 
Back
Top Bottom