Kusamehe ni kuongeza baraka maishani

Kusamehe ni kuongeza baraka maishani

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,727
Wanajamvi, ninaamini tumekuwa na w/endi njema na tulivu huku kwingineko tukihamasishana kutoa misaada kwa walioathirika na tetemeko mkoa wa Kagera.

Nia ya mada hii ni kukumbushana maana halisi na thawabu za kusamehe, ikizingatiwa na ukweli kwamba wengi wengi tunapenda kulaumu, kuomba lakini kusamehe au kushukuru hua ni kama adhabu.

Haipaswi kuhukumu mtu anapokesea, kwani kila binadamu ni dhaifu kwa namna moja au nyingine. Unapolaumu, maana yake unayemlaumu unamtenga. Jifikirie ukitengwa wewe uchungu utakaoupata!

Unapokataa kusamehe maana yake wewe hutendi makosa na ukitenda makosa nawe hutegemei kusamehewa. Ukisamehewa unakuwa na amani, na ukisamehe unapata baraka za uliyemsamehe. Lakini vijana siku hizi, kila la wenzao ni baya kwao. Wajuaji kuliko.

JE, MARA YA MWISHO ULISAMEHE, NAWE ULISAMEHEWA LINI?
 
Kweli kabsa,,,, na wengi hawajui """anaeomba msamaha ndio anapata faida kuliko anaeombwa msamaha
Ukiomba msamaha unasamehewa mara dufu, je, twajua hilo au kuomba na kulaumu tu!

JF imejaa wajuaji wa kulaumu tu! Je, twajua matokeo ya lawama hizo ndani mwetu!

Naamini unapolaumu na ikatokea ni tofauti ulivyotarajia, hujisikii vyema rohoni hasa unapokutana na uliyemlaumu
 
Tujifunze kusamehe na kusahau pia.
 
Wote nilowakosea naomba msamaha

Utaishi kwa amani sasa rohoni kama umeomba msamaha wa dhati, hata kama uliowakosea hawatakusamehe. Ila ni vizuri ukafanya hivyo kwa kila uliyemkosea.
 
Msamaha ni jambo la lazima kutoa kwa mtu aliyekukosea sio la hiari maana hata katika kitabu kitakatifu tunaambiwa jinsi Yesu alivyowafundisha wanafunzi namna ya kusali ktk sala ya Bwana kuna kipengele kinasema utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea, so usiposamehe na wewe autosamehewa hivyo msamaha kwa faida yako.
 
Kuomba msamaha ni sawa lakini sio makosa yote hutolewa msamaha mengine ni sharti utoe adhabu ndo inakuwa sawa!!! kwa maana ukisema usamehe unajua nini kitajakutokea baadae!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom