kindili kindili
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 242
- 54
Wapendwa kama nataka kusajiri NGO ...ni ngo itakayofanya kazi na shule tu ..zote za serikar na private naanzia wapi? je wizara inasajiri? nahitaji nini na nini? nifungueni macho wapendwa. Natanguliza shukrani
AU SOMA KWANZA MAELEZO HAYA, THEN CONTACT ME IN CASE YOU NEED MORE INFORMATION:-
Watu wengi wamekuwa na mawazo ya kuanzisha asasi zisizokuwa za kiserikari (AZAKI) au NGO. Ni wazo zuri kuanzisha AZAKI ila ni muhimu kutambua ni kwanini unataka kuanzisha. Watu wengi hasa vijana wanaomaliza vyuo vikuu wamekuwa na mawazo ya kuanzisha AZAKI ili waweze kujiajiri kupitia asasi hizo wanazoziasha. Sio mbaya kuwa na wazo la kuanzisha AZAKI kwa lengo la kujiajiri lakini bado sio lengo la msingi. Lengo kuu la kuanzisha AZAKI ni kushirikiana na jamii ili kutambua changamoto zinazowakabiri na kutafuta ufumbuzi.
AZAKI nyingi zimeshindwa kufanya kazi vizuri kutokana na malengo ya mwanzo ya waanzilishi siyo kuisaidia jamii bali kujinufaisha wao wenyewe. Hivyo ni vyema kabla ya kuanzisha AZAKI kutambua kwamba malengo makuu ya uanzishaji wa AZAKI ni kusaidia jamii na mengine yanafata.
Kwa wale wanaotamani kuwa wajasiriamali jamii wenye malengo ya kuleta mabadiliko katika jamii, zifuatanzo ni njia za kufuata wakati wa kuanzisha AZAKI/NGO:-
Kutambua changamoto zinazokabili jamii husika. Zipo changamoto nyingi jamii wanazokumbana nazo ila ni muhimu ukachagua changamoto ipi ungependa kukabiliana nayo, inaweza kuwa kuwasaidia watoto, walemavu, ukosefu wa ajira, kilimo, teknologia, afya, elimu, demokrasia na haki za binadamu n.k. Ni vyema ukachagua kundi lipi la changamoto unaloweza ukakabiliana na mambo mengine (mtambuka) ni kwa asasi zote zinaweza zikashiriki kutatua maswala hayo mtambuka kama mazingira, Ukimwi, utamaduni na usawa wa kijinsia.
Kuwashirikisha watu sahihi wenye mawazo yanayofanana na yako. Uanzishaji wa NGO/AZAKI ni harakati ambazo hazionyeshi faida ya kifedha ndani ya mda mfupi na wakati mwingine faida kubwa ya kifedha kwa mwanzilishi/waanzilishi isionekane kwani lengo kuu ni jamii kunufaika na siyo waanzilishi. Hivyo ni vyema waanzilishi wakawa waelewa wanao litambua hilo. AZAKI nyingi zimekufa kwa migongano ya kimaslai kati ya waanzilishi wanaodhani AZAKI ni kama kampuni na huwaza kugawana fedha hasa wanapopata fedha za wafadhili.
Andika katiba ya AZAKI/NGO. Katiba ni mwongozo unaoonyesha mambo muhimu yatakayoiongoza asasi yenu. Mambo hayo yanaweza kuwa, jina, anuani, malengo, maono, mikakati, uongozi wajibu na haki, uwajibikaji, uhasibu na fedha, utaratibu wa kuvunjika, n.k. Ni vyema ukapata mshauri akakushauri uandishi wa katiba ya asasi ili kupunguza makosa yatakayosababisha usumbufu wakati wa usajiri.
Washirikishe viongozi wa kata. Ni vyema ukawashirikisha uongozi wa kata wakakupa barua ya kuwatambua.
Baada ya kupata barua ya kuwatambua, barua hiyo utaipeleka katika ngazi ya wilaya/manispaa kwa afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ambaye atakupa barua ya utambulisho pia.
Barua ya utambulisho utakayoipata, utaipeleka kwa afisa maendeleo wa mkoa ambapo afisa maendeleo wa mkoa atakupa barua ya kukutambulisha wizara ya maendeleo ya jamii na vilevile utajaza fomu na.1.
Usajriri unaweza ukafanyika katika wizara ya maendeleo ya jamii au wizara ya mambo ya ndani. Taratibu za usajiri wizara ya maendeleo ya jamii baada ya kufuata taratibu hizo hapo juu, ni:-
a)Nakara tatu (3) za katiba
b) Muktasari wa kikao cha waanzilishi waliopendekeza uanzishaji wa AZAKI/NGO pamoja na saini za waanzilishi
c) Wasifu/CV na picha mbili za watendaji wakuu watatu wa ofisi.
d) Anuani na mahali ofisi ilipo.
e) Ada ya uanzilishi
f) Na viambatanisho vingine kadri vitakavyoitajika na msajiri.
Gharama za usajiri
Gharama za usajiri katika ngazi ya wilaya ni Shs 41,500/= ambapo:
- Gharama ya ujazaji fomu Shilingi 15,000/=
- Gharama ya usajiri Shilingi. 25,000/=
- Stamp duty ya TRA 1,500/=
Gharama ya usajiri katika ngazi ya mkoa Shs 56,500/= ambapo:

- Gharama ya usajiri Shilingi 40,000/=
- Stamp duty Shilingi 1,500/=
Gharama ya usajiri ngazi ya taifa Shs 66,500/= as follows:
- Ujazaji fomu shilingi 15,000/=
- Usajiri shilingi 50,000/=
- Stamp duty shilingi 1,500/=
Gharama ya usajili katika ngazi ya kimataifa USD 267 ambapo:
- Ujazaji fomu USD 15
- Usajiri USD 250
- Stamp duty USD 2
Ni vyema ukajipanga kwa kuwa na nakara hizo muhimu na fedha ya kulipa gharama kama zilivyoorodhesha hapo juu ili ufanikishe usajiri wako bila usumbufu wowote
Karibu katika ulimwengu wa kupambana na umaskini kwa kuleta mabadiliko chanya katika jamii!!!!
NAKUTAKIA KILA LA HERI KATIKA HUO MCHAKATO WAKO...

Shukrani saana mkuu mi nimekuelewaa saana Mungu akubarikiAU SOMA KWANZA MAELEZO HAYA, THEN CONTACT ME IN CASE YOU NEED MORE INFORMATION:-