Wakuu naomba mrejee kwenye kichwa cha uzi.Nina laptop nataka niitume Songea,naomba mwenye kujua watu wanaofanya hii kazi na ikiwezekana na gharama zao.Nipo dar
wakuu naomba mrejee kwenye kichwa cha uzi.nina laptop nataka niitume songea,naomba mwenye kujua watu wanaofanya hii kazi na ikiwezekana na gharama zao.nipo dar
mara nenda ile magari yanapofika mkabizi dreva au konda kisha mpe posho yake chukua namba,hakikisha unaenda ofisini kuomba namba ya dreva na jina lake kabla gari haijafika,ili ikifika unalinganisha namba na jina unakuwa na uwakika
Secret Star usimwogopeshe mwenzio bana huyo mtu unayemjua akikwambia kuwa ameibiwa kwenye basi utamdai? mbona kila siku tunasafirisha vitu vya thamani na vinafika popote tanzania kwa kutumia haohao unaowaita wezi? Ze Heby hiyo laptop usimpe dereva wala conductor, ifunge vizuri ipeleke kwenye Ofisi za Super Feo Express, Shule ya Uhuru jirani na ofisi za Kampala Couch (usipeleke ubungo, mizigo yote ni ofisi ya kkoo), ikabidhi pale na uwaambie wazi kuwa ni laptop (for extra care), utaandikiwa risiti inayoonesha umesafirisha laptop, bei ni 20,000/- (elfu ishirini) kwa laptop moja. Ondoa shaka mzigo wako utafika salama salmini, usisahau kuandika jina na namba ya unayemtumia juu ya parcel, pia hakikisha kuwa ana kitambulisho atakachowasilisha siku ya kuchukua mzigo.