GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nimelitafakari kwa siku nyingi sana hili jambo kwa marefu na mapana yake hasa nikizingatia kuwa sasa tupo katika dunia ambayo Uchumi wake ni mbaya na maisha kiukweli ni magumu kiasi kwamba hakuna unafuu wowote sana sana ni mateso tu.
Nimekuwa nikishuhudia baadhi ya Familia zikiwa zinatumia rasilimali zake nyingi tu hasa katika kumuuguza Ndugu yao / Mpendwa wao ambaye kimsingi huja kufariki baadae huku akiwa tayari ameshaitia hasara kubwa sana ile Familia.
Kwa maana hiyo maani leo nimeona nililete hili jambo humu kwenu wana JF kuwa hivi kwa maslahi mapana ya Familia fulani huku hali hii ya maisha ikiendelea kuwa ngumu siyo jambo la busara endapo ukiwa na Mgonjwa wako ambaye akishapimwa na kuonekana kuwa Ugonjwa wake hawezi kupona basi kuliko kuwapotezea muda na rasilimali Wanafamilia, Ndugu na Jamaa basi tusipotezeane sana muda na Madaktari waruhusiwe tu kuwapiga Sindano za Sumu ili wawahi Kufa tumzike na maisha yaendelee?
Kwa mfano hivi kuna tija gani mnajua kabisa kuwa mgonjwa wenu amegundulika na Saratani fulani au ameathirika tayari na Dally Kimoko ( VVU/UKIMWI ) au Figo imeshakengeuka na hawezi tena kupona halafu bado Watu tunaendelea kuwauguza huku tukitumia hadi kile kidogo tulichokihifadhi Benki?
Hivi haitokuwa na Tija kama huyu Mgonjwa akipewa tu Sumu atuache au atupishe duniani kusudi hizi Pesa au Rasilimali zilizopo za Wanafamilia wake zitumike kuiendeleza Familia yake kwa manufaa yao ya baadae kuliko kuitumia yote kumuuguza Yeye kwa muda mrefu halafu akishafariki tu Wanafamilia wanakosa hata Hela ya Kununulia Jeneza, kusafirisha Mwili wake kwenda kumzika na anaiacha Familia au Wana Ukoo wake katika Umasikini uliotukuka?
Naomba kuwasilisha na asubuhi njema nyote.