Kurudisha Umitashumta pekee haitoshi kuinua michezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kurudisha Umitashumta pekee haitoshi kuinua michezo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 28, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  BAADA Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kurudi michezo kwenye shule za msingi nchini Umitashumta yaliyomalizika hivi karibuni Kibaha, Pwani na Mbeya kutwaa ubingwa katika mchezo wa soka.

  Kurudishwa kwa michezo hii kwa sasa ni ishara njema kwa maendeleo ya michezo hapa nchini na nikiamini kwamba Waziri Dk Shukuru Kawambwa atakuwa tayari kushirikiana na wadau wote katika kufikia malengo ya dhati.

  Lakini jambo la msingi ni serikali ilitakiwa ielewe kwamba bajeti inayoelekezwa kwenye michezo ihusishe matumizi na matengenezo ya vifaa vya michezo.

  Katika kuhakikisha michezo inatengewa bajeti ya kutosha na inaendelezwa nadhani waziri wa afya, waziri wa elimu na waziri wa michezo wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja ili kufanikisha hilo. kwa sababu hapa kuna suala la elimu ya mazoezi ya viungo na elimu ya afya huku wote tukielewa michezo ni afya.

  Ni rahisi kukuza elimu kwa vijana kupitia elimu ya mazoezi ya viungo na michezo kwa ujumla.

  Ni lazima tuelewe umuhimu wa elimu ya mazoezi ya viungo katika mashule.

  Lazima tukubali wachezaji nyota katika mchezo wowote huandaliwa, lakini bado tatizo kubwa la maendeleo ya michezo nchini likiwa ni maandalizi ya wanamichezo wetu na hakuna shule maalum za michezo zilizoanzishwa na serikali,mfano Makongo sekondari.

  Nataka kumshauri Dk Kawambwa baada ya kukubali michezo hiyo mashuleni hipo haja ya kutafuta walimu wamichezo ambao watakuwa wakiendelesha gurudumu hilo katika maeneo ya shule kama ilivyokuwa zamani.

  Naamini nia ya Rais Jakaya Kikwete kutaka kufufua michezo haitoweza kufikiwa kama shule hizi zitakosa walimu na mtahala wa michezo wenye kueleweka.

  Pamoja na kukubaliana na uamuzi huo, lakini tunapenda kushauri yafanyike mambo kadhaa ya kuyafanyia kazi kama kweli serikali imedhamiria kurejesha michezo kwa vijana.

  Kwanza, naishauri irejee sheria na kanuni zinazosimamia michezo kwa lengo la kuifanya iwe yenye maana kwa watoto wetu.

  Katika hili, nashauri iainishe ni jinsi gani suala hili litaweza kufanyika katika shule zetu, zikiwamo za mijini na vijijini ambazo zimejengwa katika maeneo ya kuchezea yamemegwa au kuuzwa na wajanja wachache wakiwamo wale walioko serikalini.

  Kwa hili, nashauri wale waliogawiwa maeneo ya wazi na yale yaliyokuwa yametengwa kwa shughuli za michezo ama waondolewe na kupewa maeneo mengine, kama watakuwa wamemilikishwa.

  Pili, nashauri zitungwe kanuni ambazo zinafanya siku moja kwa wiki inakuwa maalum kwa michezo, kama ambavyo imekuwa ikianyika katika shule za binafsi, au zile ambazo zinajiita za mchepuo wa Kiingereza (English Medium), ambako michezo imepewa umuhimu mkubwa.

  Tatu, nashauri kwamba suala la kufundisha walimu katika vyuo vya ualimu kwa ajili ya kufundisha michezo, lakini nalo halina budi kuangaliwa ili kuondoa uwezekano wa wahitimu kujikuta wakifanya kazi nyingine badala ya kufundisha michezo katika shule zetu.

  Nne, nashauri michezo baina ya shule zetu, kwa maana ya Umitashumta, kwa shule za msingi na Umisseta, kwa shule za sekondari, ipewe mtazamo mpya.

  Itakumbukwa kwamba michezo hiyo ndiyo iliyokuwa chimbuko la wachezaji ambao baadaye walitokea kuwa wanamichezo wazuri waliolisaidia taifa kitaifa na kimataifa, miaka ile ya sabini hadi mwishoni mwa themanini.

  Kwa maana hiyo, nashauri michezo hiyo ifufuliwe kwa kuangalia mahitaji ya jamii kwa sasa, kwani haitakuwa na maana kama tutawaandaa wachezaji kutoka shule za msingi, sekondari, lakini baadaye wanaachwa kuozea mitaani.

  Tano, ushauri wangu ni kuifanya michezo kuwa ya uweledi na wanamichezo waweze kujipatia kipato chao huko kama ilivyokuwa kwa sekta nyingi hapa nchini.

  Kwani kwa kuifanya michezo kuwa ajira kamilifu na kuachana na dhana ya sasa ya kuwa michezo ni ridhaa na si ajira ya kuitegemea, ndio maana wachezaji wengi wanatumika na kuwa nasifa kubwa lakini wanapostaafu au kuumia maisha yao yanapotea kabisa.

  Pia, kuangaliwa kwa mfumo ambao uliwapa nafasi wanamichezo kupata ajira katika taasisi za umma na ubinafsi, yakiwamo majeshi yetu ambako kwa sasa shughuli za michezo zimedorora au kuachwa.

  Kwa maana hiyo, tunaamini kuwa wakiandaliwa wanamichezo wetu kutoka utotoni, kisha kuachwa mitaani baada ya kumaliza shule, maana halisi ya kurejeshwa kwa michezo itakuwa imepotea.

  Nashauri kwamba, kama alivyoeleza Rais Kikwete, klabu zetu nazo zishauriwe kuangalia suala la wanamichezo hao walioandaliwa, wasiachiwe tu kujifunza michezo katika shule na vyuo, kisha watumiwe kuisaidia nchi yetu kupiga hatua katika michezo ambako tumepoteza dira na mwelekeo.

  Jambo jingine ambalo tunashauri lifanyike kuhusu michezo ni kuangaliwa michezo mingi zaidi badala ya soka, kama ambavyo imekuwa mazoea katika nchi inapozungumziwa michezo.

  Sote ni mashuhuda wa jinsi ambavyo michezo kama riadha, kikapu, ngumi inavyoweza kusaidia kuitangaza nchi yetu kimataifa kama itapewa msukumo na mtazamo mpya kupitia mwamko huu wa sasa wa kurejesha michezo.

  Nadhani, kama haya yatazingatiwa, basi Tanzania itakuwa imeanza kuona mwanga na pengine miaka michache ijayo itakuwa tayari kwa michezo ya kimataifa kama Olimpiki ambayo kuanzia mwaka 2012 kule London, Uingereza na inayofuata, tutakuwa tumepata wawakilishi wazuri na walioandaliwa kushindana.

  Napenda kuwapongeza wafadhili kutoka Finland ambao wamewekeza katika mradi huu wa kufundisha walimu wa michezo, lakini tunatadharisha kuwa fedha zao zinafaa zitumike vizuri na kuiletea nchi yetu tija, kupitia michezo.

  Vinginevyo itakuwa ni kuwabebesha mzigo wa madeni wa kulipa mikopo hiyo Watanzania kwa mipango ambayo haina maana wa tija.
   
Loading...