Naombeni ushari wana JF.
Mimi niliajiriwa 2004 na JWTZ kama askari baada ya kumaliza form four. Nilifanya mtihani wa form six nikiwa jeshini na kufaulu vizuri, Nikatamani sana kuendelea na elimu ya juu. Nilijitahidi kuomba ruhusa kikosini ilishindikana, nilifika makao kuomba msaada nikakuta msururu mkubwa wa maombi haujajibiwa kwa miaka kadhaa nyuma. Nikaamua kuomba chuo nikapata, Nikaomba mkopo nikapata asilimia mia, Ruhusa nikaikosa. Nikaamua kuacha Jeshi. Nilianza chuo 2009 nikamaliza 2012.
Natamani kurudi jeshini, nilifika Makao makuu nikawaona wanasheria wakaniambia ni vigumu mimi kushinda kesi labda kama nitakuwa na mtu mkubwa kunisaidia. Wana JF msinihukumu kwa makosa niliyoyafanya nisaidieni mawazo.
Karibuni