Kura ya maoni March 30 2015, Daftari kuboreshwa kwanza

Kura ya maoni March 30 2015, Daftari kuboreshwa kwanza

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,487
Reaction score
39,965
Hatimaye mwana sheria mkuu wa serikali Fredrik Werema amesema kuwa kura ya maoni itafanyika tarehe 30/03/2015.

Aidha kampeni zitaanza mwezi wa tatu mwanzoni na daftari la wapiga kura litaboreshwa kwanza.

Aidha katika sintofahamu iliyojitokeza ni kuwa kutakuwa na mabadiliko ya sheria ya kura ya maoni kwenye bunge lijalo ambapo swala la uchakachuaji wa theluthi mbili ya kupitisha katiba huenda likafanyika na kugeuzwa kuwa katiba ipitishwe kwa wingi wa kura.

Kwa maelezo zaidi fuatilia gazeti la leo la MWANANCHI.
 
Kaka Nape anawamalizia waandamanaji teh teh viroba vimeshindwa...sisi tunauza sera nyie mnauza viroba
 
... Hiyo Itakua Katiba Ya Ccm, Katiba Ya Watanzania Bado.!
 
... Haraka Ya Nin, Au Wanataka Ionekane Kwamba Jk Ndo Alieanzisha Na Kamaliza
 
Katiba Mpya haikuwa ni sera ya Maccm.

Mnawaza mambo ya Chadema
Naona mfalme Mbowe atakuwa kafurahi sana alichokuwa anakitika serikali sikivu imekifanya itaboresha kabla ya kura.
 
Naona mfalme Mbowe atakuwa kafurahi sana alichokuwa anakitika serikali sikivu imekifanya itaboresha kabla ya kura.

Machakachuaji naona yameanza tena mbinu chafu!
 
Machakachuaji naona yameanza tena mbinu chafu!
Nyie pro-Chadema viumbe wa ajabu sana juzi kiongozi wenu Mbowe kabla hawajaenda Oman na Lukuvi, alitoa tamko kuwa watazunguka nchi nzima kupinga kura ya maoni kufanyika bila kuboreshwa taftari kwanza, leo kilio chenu kimesikilizwa bado mnalalamika tena.
 
Mbona mnataka kuchakachua sheria ya kura ya maoni?
 
Daftari likashaboreshwa haisadii kitu.
Kura ya maoni hakuna wwangalizi wala mawakala wa vyama .
Huko ni tume tu.wakiamua kuchakachua watafanya tu na hakuna sheria ya kuhoji.ndio maana ccm wanasema wataipitisha tu
 
Binafsi naona hii imekaa vizuri, ni bora kura ya maoni ikapigwa mapema kuliko kusubiri mpaka baada ya uchaguzi. Watanzania tunajijua ni watu wa kusaahau haraka na kupuuza kila kitu Hivyo ni bora kura ya maoni ikafanyika mapema ilingali hasira za wananchi juu ya uchakachuzi wa maoni yao waliyoyatoa ktk Tume ya Warioba haijapoa, So naunga mkono hoja.

Cha msingi wananchi waelimishwe juu ya umuhimu wa Katiba mpya iliyotokana na maoni yao na wahamasishwe wajitokeze kwa wingi kujiandikisha pindi wakati utakapofika ili waweze kutumiza wajibu wao wa kuikataa rasimu hii iliyotokana na mawazo ya mafisadi kina Chenge na washirika wao

Tujitokeze kwa wingi kuandikishwa

BACK TANGANYIKA
 
Hatimaye mwana sheria mkuu wa serikali Fredrik Werema amesema kuwa kura ya maoni itafanyika tarehe 30/03/2015.

Aidha kampeni zitaanza mwezi wa tatu mwanzoni na daftari la wapiga kura litaboreshwa kwanza.

Aidha katika sintofahamu iliyojitokeza ni kuwa kutakuwa na mabadiliko ya sheria ya kura ya maoni kwenye bunge lijalo ambapo swala la uchakachuaji wa theluthi mbili ya kupitisha katiba huenda likafanyika na kugeuzwa kuwa katiba ipitishwe kwa wingi wa kura.

Kwa maelezo zaidi fuatilia gazeti la leo la MWANANCHI.

Inasikitisha sana kwenda kupiga kura ya maoni kupitisha "HARAMU".
 
Back
Top Bottom