Zanzibar 2020 Kura kwa Dkt. Mwinyi; Chagua ilani bora, chagua umeme wa uhakika

Sep 8, 2020
66
125
Kwa kipindi cha miaka mitano ijayo (2020-2025), CCM itaielekeza SMZ kufanya mambo yafuatayo kwa ajili ya UMEME na NISHATI mbadala Zanzibar;

1. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati ya Mwaka 2020 na kuendeleza juhudi za upatikanaji wa umeme na nishati mbadala.

2. Kuimarisha shughuli za usimamizi wa huduma za umeme na usambazaji wa nishati katika vijiji 305 (Unguja 180 na Pemba 125).

3. Kujenga njia kubwa ya umeme ya msongo wa 132KV kwa kuelekea kusini na kaskazini mwa kisiwa cha Unguja yenye urefu wa kilomita 100 pamoja na kujenga vituo vikubwa viwili vya kupoza umeme kwa lengo la kuimarisha huduma bora ya umeme.

4. Kuimarisha miundombinu ya usambazaji umeme wa 11 KV kwa Unguja.

5. Kufanya utafiti wa vyanzo vya umeme pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa jua ili kupata umeme wa Megawati 30 kwa Unguja na Megawati 8 kwa upande wa Pemba.

6. Kuimarisha Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kwa lengo la kuliwezesha kujiendesha kibiashara.

7. Kuwapunguzia wananchi gharama za uungaji umeme kwa watu wenye kipato cha chini.

8. Kufanya utafiti wa kina wa mlinganisho (Comparative Study) wa kuwezewesha kupata chanzo kipya cha nishati ya umeme ili kukidhi mahitaji ya ziada yanayojitokeza.

9. Kuanza ujenzi wa bohari yenye uwezo wa kuweka tani 30,000 za mafuta ya petroli katika bandari mpya ya Mangapwani kwa ajili biashara ya mafuta na gesi.

10. Kuhamasisha matumizi ya majiko banifu na kushajiisha matumizi ya gesi majumbani, viwandani na vyombo vya usafiri ili kupunguza matumizi ya makaa na kuni kwa ajili ya kulinda mazingira.

11. Kushajihisha sekta binafsi kuwekeza katika usambazaji wa nishati ya mafuta na gesi.

12. Kuhamasisha uwekezaji wa huduma za vyombo vya usafirishaji wa mafuta na gesi (supply vessels).

CHAGUA ILANI BORA, CHAGUA UMEME WA UHAKIKA.
#KuraKwaDR.Mwinyi,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom