Kuporomoka kwa Beit al Ajiab

Kuporomoka kwa Beit al Ajiab

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,492
Reaction score
33,051
KUPOROMOKA KWA BEIT AL AJIAB ''IT HAS BEEN A LONG TIME COMING''

Kuanguka kwa Beit Al Ajiab ni kilile cha kile ambacho kwa hakika kimechelewa sana kutokea.

Kuna mtu mmoja kaniandikia ujumbe ananiomba haraka nifike Zanzibar nikaangalie mifupa ya watumwa waliozikwa kwenye nguzo za jengo lile na akasisitiza nisifanye ajizi nikapitwa na fursa hii adhim.

Bad taste.

Maskahara kwenye janga kubwa na zito kama hili hayafai.

Lakini huyu ndugu yangu nimemuelewa.

Picha hizo mbili hapo chini nimezipiga Pangani kiasi cha miaka 10 iliyopita wakati niko na Dr. Harith Ghassany akifanya utafiti wa kitabu chake maaruufu ''Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni.''

Nimeongeza na picha nyingine mbili moja ya Bushiri bin Salim (na ningependa msomaji asome maelezo yaliyopo kwenye picha hiyo) na picha ya Sultani Barghash bin Said aliyejenga Beit Al Ajiab.

Wakati tunatembea katika mitaa ya Pangani tulikuwa tunashuhudia utajiri wa majengo ya zamani yanayoonyesha historia ya Tanzania, majengo ambayo yalikuwa yanaporomoka kwa kukosa matunzo.

Majengo haya ukipenda unaweza kuyaita magofu kwa kuwa hayakuwa yanakaliwa tena.

Nilitambua haraka sana baada ya kupita kote kuwa wapo watu kwenye madaraka na nafasi ya kufanya maamuzi hawakuwa na mapenzi na historia hii.

Nilithibitisha hili pale nilipojua kuwa waliokuwa katika nafasi zile hapo Pangani hawajui hata kaburi la shujaa Bushiri bin Salim Al Harith liko wapi.

Hawajui kaburi la shujaa aliyepigana na Wajerumani kuitetea nchi yake liko wapi.

Kwao wao Abushiri hana umuhimu kama majengo yale yalivyokuwa hayana umuhimu yakaachiwa yameguke kidogo kidogo hadi yatoweke na historia yote ya watu hawa ipotee kabisa.

Beit Al Ajiab limechelewa sana kuanguka.

IIa sielewi kwanini lilichagua siku hii na muda huu kuanguka.

1609001384659.png

1609001522402.png
 
Back
Top Bottom