PostGE2025 Kupitia jicho langu siku ya October 29, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

MaweSaba

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2024
Posts
382
Reaction score
568
Majira ya saa tisa alasiri, moshi ulionekana kweli viunga mbali mbali ndani ya jiji la Dar Es Salaam.

Wakati polisi wanaanza kufyatua Risasi... watu wengi hawakuwahi fikiria serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ingewahi agiza polisi wamimine risasi hovyo kwa raia waliokua barabarani njia ya kuelekea Gongo la mboto.

Mwanzo watu wengi walidhani rubber bullet zinapigwa kuzuia watu... kumbe haikua hivyo.

Mida ya saa kumi kijana mmoja mfanyabiashara wa soko la kipawa alipopatwa na risasi tumboni na utumbo kutoka, vijana wengine wakiwa na pikipiki wakikimbia kutoka Vigunguti gari la polisi aina ya Land Rover lilipita kwenye makutano ya Jet na kumimina risasi kwa vijana waliokua service road wakielekea airport.

Hapo ndipo hofu, mshtuko na uhalisia ulitupata, nchi yetu kwa mara ya kwanza tunaanza kushuhudia mauaji ya mwanzo kwa macho yetu...

Siku mtandao unarudi, depression ilitupata kwa picha za vijana na story za watu walivyo uawa kikatili

Itaendelea
 
ok.
Inna lillahi wa inna illayhi rajir'un 🐒
 
Lowasa alikuwa mbele ya muda sana, fikiria 2015 angeruhusu watu waingie barabarani na watu kufa kisa urais yeye aliamua bora akose huo urais na maisha yaendelee leo mbaya wake ndiye amasababisha watu kuuliwa oct29
 
watu zaidi ya million 20 ni mashahidi, kila mmoja aliona chake
Sina shaka na hilo,shaka ni kwamba inawezekana watu wa Jaji Chande na Samuya wanapita. Humu wanatafuta habari zaidi ili waweze kuharibu ushahidi.
Shida ni kwamba utamjuaje mtu mwema na mtu ajenti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…