Chimwemwe tajiri wa kike
Member
- Aug 4, 2019
- 20
- 56
Moyo wangu unaumia sana una kidonda nimempenda mtu ambaye hana mda na mimi. Iko hivi, tumejuana miaka 9 kama marafiki kipindi chote alikuwa ananitaka ila si kuona muda muafaka, na si kutaka kupoteza pia nami nilikuwa nataka nijipange kwanza ndo niwe naye. Well akapata wadada wawili na wamezaa nae mmoja wa kike mwingine wa kiume kaachana na wote.
Mwaka huu nikasema niwe naye, nikimfata nauli ya uber nalipia mwenyewe kama gari najaza mafuta mwenyewe, yeye hajiongezi kama mwanaume. Nina kazi yangu najimudu naye ana kazi nzuri zaidi yangu mie, kipato mara 7 zaidi ya cha kwangu. Hapo kutuma msg mpaka mie nianze, nikipiga wakati mwingine hapokei, najua anakuwa busy na kazi ila hawezi kosa dakika chache za kunipigia, najikuta naumia sana.
Namuwaza nampenda ila naona yeye bado ana umwana mwingi na mimi anaendelea kunichukulia kama mshikaji badala ya mpenzi. Nawaza au sababu mwenzangu ni PhD holder? Au sababu yeye ni familia bora na mie nimetoka usekweni?
Leo nimemblock WhatsApp hapa moyo unaniuma sana yaani naumia sana najikaza.
Tafadhali marafiki nipeni mawazo yenu nsimuunblock wala kumtafuta na akintafuta nsimsikilize.
Ee Mungu wangu naomba unipe mwanaume uliyemuandaa kwa ajili yangu, natumia hajafariki kwenye moto Morogoro.