Kupenda ni kuiona thamani ya mtu uliyenaye/unayemtarajia

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Mahusiano ya kimapenzi ni kupeana thamani, unapofanya maamuzi ya kuwa na mwenza ina maanisha yeye ni bora kati ya wengine. Maamuzi haya sio ya kukurupuka au kusukumwa na marafiki, ndugu ama jamaa zako inapaswa uwe ni wewe mwenyewe. Unapochagua mwenyewe kuna faida yake ikiwemo, pale unapokushindwa kuubeba mzigo wako ni rahisi kuushusha.

Swali gumu unaionaje thamani kwa mtu uliyenaye au unayemtaraji, tafakari kwa haya:

Upekee unaona anao tofauti na watu wengine, wakati mwingine mtu aliyetendwa katika mapenzi, hapa huwa ni mteremko maana tayari huwa na mzani wa kulinganisha yaani yule alopita na huyu mpya.

Kwa anayeanza mahusiano yeye anapaswa kujitazama yeye kama yeye kitu gani au maisha yake anayotaka yawe na anayehusiana nae wanaenda sawa, anapaswa kuangalia jamii yake inayomzunguka maisha ya mahusiano kitu gani kwao ni kipaumbele na yanafurahisha hata kama ni familia kwa kujifunza kwa wazazi wako ama walezi.

Upekee wa mtu ndio huwa kilema cha mtu kabaki nawe, iwe ni kimwili, kiakili, kiafya, kimahitaji au kiutafutaji. Tazama jamii, kuna mtu watu wakimwona tu wanamnyoshea vidole " bhana ni waifu matilio " anafaa kuwa mke" au " yule ni bonge la bwana" " yule ni kicheche ila dah huwezi jua", tazama wapo wanaogombana mara kwa mara, wapo ambao mmoja kati ya wenza ni mtu mwenye tabia za ajabu ila mwenzie anatambua na kwake halimpi shida, sio bure kuna cha upekee anacho anacholingia.

Nafasi anayokupa mwenza wako unapohusiana na mtu itazame nafasi anayakopa katika ratiba zake na maisha kwa jumla, anayependa huwa yuko tayari hata ratiba imbane namna gani ataitafuta hata sekunde ya kukupa nafasi ili ujue yupo kwa ajili yako, kuna mtu hawezi hata kukutetea chochote kukuzingatia kwa lolote, kuna zile meseji unamtumia mtu hata kumjulia hali yani mpaka unajuta.

mfano;
Juma: umeamkaje?
Asha: poa.
Juma: vipi leo nitakuona?
Asha: sijui.

Hapa ni tatizo ni kama unalazimisha mapenzi kwa mtu aliyesema anakupenda na kama ni pozi basi ni pozi povu. Suala la kukutambulisha kwa marafiki, ndugu au kuambatana nawe huwa hawezi, kama hajakuoa hata gheto kwake kukufiisha anaogopa. Mmh sio bure tafakari.

Kukuheshimishwa Kwa namna yoyote ile anakuwa ni mtu wa kutaka upewe heshima yako stahiki, ukiwa na mtu asiyefanya mambo kwa kutunza heshima yako, kukutusi hadharani/kwa marafiki, anakuendesha awezavyo kama gari ya mkoloni, ebwana ee! Hapo tafakari.

Kuheshimiana ni moja ya stara kwa umpendae, wapo watu waajabu picha za utupu za mpenzi wake au mwenza wake anaziweka hadharani au kwa washikaji kama vile stori ya kawaida, hapana tafakari huyo mtu hana afya ya akili.

Kukujali kama wajibu wake sio kwa kuombwa ombwa Utamaduni wetu waafrika kila jinsia ina majukumu yake kwa mwenzie, mkishakuwa katika mahusiano ni suala la kila mtu kujua nini anapaswa kumtendea mwenzie, sio suala la kukumbushana.

Unapokuwa na mtu unayemkumbusha mara kwa mara, tafakari. Endapo mmezidiana uwezo, basi hakuna jipya zaidi ya kusaidiana, wapo wanawake wanauwezo kushinda waume zao, sasa isiwe wewe ni Mbunge alafu jamaa ni fundi gereji, ila bado bili zote akomae nazo na ada kisa ni mwanaume, huku sio kupeana thamani ni kukomoana.

Kukuamini wewe kwanza ndio wengine wafuuate mahusiano yana namba chache ya watu ni wawili, suala la kuaminiana ubaki kati yenu na sio nje ya watu wawili, anayekuhukumu kwa kuambiwa, anayemsikiliza sana mwingine kuliko wewe uliyenaye ni tatizo. Mfano kuna mwenza anampa ushauri mwenza wake, ila akitoka hapo anakutana na mwingine anampa ushauri na kuyababe yale bila hata kumshirikisha anafanya huu ushauri mpya, likiharibika "si fulani aliniambia", hapana tafakari. Thamani ya mtu wako unaishusha.

Ubinafsi mtu anayekupa thamani anataka ufanikiwe, uwe na afya, uwe na akili timamu, uwe na kila kitu muhimu cha dunia, hawazi yeye apate wewe ukose na hata akiwa amebarikiwa kingi kuliko wewe yuko tayari kula nawe. Iwe ni kujenga, makazi, biashara, ndoto ama chochote kile kitabakia kuwa kati yenu ni chenu kuna mwenza ukiwa na furahi ni yakwenu wote, ukiwa na shida ni yako pekeako.

Hapana, tafakari.
Hana papara wala mchecheto na wewe Kila anachokifanya ukifikiria matokea yake, kama ni kujamiana yuko tayari kwa matokeo, kama ni kuhusiana nawe na hajaoa au kuolewa anajua kinachofuata, kama ni mume na mke anajua kilichopo katika maisha, huwa sio muoga wa maisha, kusemezana, kukuambia mipango yake, huwa ni mtu wa kufanya lolote ila lenye tija ya maisha yenu.

Ukiwa na mwenza hupaswi kuwa na papara nae utaharibu ama atakuhararibu mana hatokuwa mtu wa kujipanga kwa lolote, atakufanya kama mpira wa kona. Thamani ya mtu huwa ni kama tambaa la deki hata liweje kazi yake italifanya lifuliwe, lisafishwe na lianikwe, litunzwe mahali litapojulikana lipo na kila mtu atalijua umuhimu wake hata awe mgeni, hata kama limetoboka na kutoa harufu umpa mtu mazoea ya kuliona ni safi na ndio linalomfanya moyo wake na akili yake kila anapoliona, kulitumia na kulifua, kwani linalomsitiri, mengine ni mbwembwe tu.

#imarika#mnogeshe umpendae#
Mwandishi: mmmuhumba
 
Mapenzi. The essence of humankind!

Hayanaga mwongozo.....

Yalishakataa kuundiwa fomyula.....

Kila couple na mapigo yake.....

Mwelewe mwenzi wako....

Kijue kimfurahishacho na kitende hicho tena kwa heshima, kujituma na bashasha tele!

Nyingine zote mbwembwe tu za motivesheno spikazi na wanasaikolojia uchwara ....

Na akiwa na tako mvumilie hata kama ana mapungufu kiasi gani 😁😁😁🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom