usihofu mama, iko namna hii,
Nyumba ina sehemu kuu 3
sehemu ya kwanza ni msingi
sehemu ya pili ni boma na
sehemu ya tatu ni paa
kati ya hizo sehemu kuu 3 sehemu ya msingi na sehemu ya paa ni part 2 zinazohitaji umakini sana na zinakuwa na gharama kubwa kidogo,
sehemu ya paa ni part inayotumia skilled labour na ni sehemu yenye risk,
mbali ya swala la kiufundi, paa kwenye nyumba ndo linaweza kubadilisha nyumba iwe nzuri au iwe mbaya,
sasa natoa mfano tu wa nyumba ndogo ya vymba 3 vya kulala, sitting room, dining, kitchen na store jumlisha veranda zote za mbele na nyumba, chukulia mfano hiyo nyumba ina jumla ya ukubwa wa 140sqm,
kutegemea na aina (design) ya hiyo ramani na paa lake labda paa lina ukubwa wa 270sqm
mahitaji ya kupaua mfano wa hiyo nyumba yapo kama ifuatavyo.
1), mbao za dawa, hasa mbao nzuri ni za SAO HILL, kama bati litatumika la Industrial Trough (I.T) (hilo ni bati la migongo mipana, manake mbao za papi hazitakuwa nyingi kama mbao za makenchi, hapo kwa SAO HILL ukubwa wa nyumba kama hiyo (tunayo'assume) jaribu kutenga pesa isiyopungua 3m za mbao tu
2), Bati kama nilivyoainisha hapo juu ni I.T mfano na running meter ni 270 , kwa mabati ya ALAF ya IT gauge 28 wanauza kwa meter moja 13500/= kupitia agent, bila agent ni 13800/= manake ni kwamba bati tu hapo litagharimu karibia 4m
3), kofia na valley labda zipo jumla 40, kofia moja wanauza 21,000/= (hizo ni kofia zenye urefu wa 3m,
manake kofia na valley zinaweza kugharimu karibia milioni moja
4), mengineyo kama misumari ya kupigia makenchi, misumari ya bati, usafiri vyote kwa pamoja weka milioni 1
5), ufundi (tafuta local fundi) labda akakufanyia kwa bei ya 2m,
ila ukumbuke local fundi akija anaagalia nyumba imejengwaje na anabuni tu namna paa litakavyokuwa na si kwa kuffuata ramani inaonyeshaje, tarajia makosa mbali mbali hapo, ila pia na ushauri atakaokuwa anakupa local fundi ujue unaweza kukugharimu wewe baadae nakubaki kulalamika kuwa nilishauriwa hivi na fundi,
kwa maelezo zaidi ni'PM email yako ntakutumia sample za ramani na budget zake na ukipenda unaweza kuzitembelea kama upo hapa dar, au mwanza, arusha na moshi,
Nyie mnafanya masikhara na paa,jamaa yuko sahihi kabisa,mi nimegonga paa imekula karibu mil 22,nyumba ya mita 17 kwa 21,nimepiga bati ya Kigae ya Jeshini mbao tu imekula 8M,Bati 6M,kofia 1.2 M,Misumari special ya Bati 0.7M,Misumari ya kawaida ya mbao 0.5M,Kofia na Valley 1.2M,Usafiri na Vibarua kwenye mbao,bati,kofia na valley jumla 1M,Ufundi 2.8M.
Msilalamike sana upauaji unategemea mambo mengi kwa mfano ukubwa wa nyumba,aina ya bati,idadi ya mbao,ramani ya paa etc,kwa mfano mtu aliyepiga bati la kawaida,bati la migongo mipana,bati la kigae na kigae hawa lazima watofautiane bei,vilevile bei ya mbao na ufundi wa bati la kigae na bati la kawaida haiko sawa bati la kigae linakula mbao nyingi zaidi,ukubwa wa nyumba ya sqm 140 hauwezi kuwa na gharama sawa ya upauaji na nyumba ya sqm 240, vilevile ramani za paa nyingine ni very complicated kwamba upauaji wake ni mgumu sana hauwezi kuwa bei sawa na mgongo wa tembo,sijui kama mnanielewa?ila kama hamkubali sio kesi nadhani kuna ambao wanaweza kunielewa hata kwa mbali sina la ziada ni hayo tu.
,nyumba ina ukubwa gani? hata hivyo andaa fedha za mbao treated timber kama 3.5m na bati 5m na ufundi 3m, kama hujapata fundi ni PM nije nicheki site then tutaongea.
Mkuu nimejaribu tu ku'assume nyumba yake ya kawaida around 120sqm to 140sqm na bati la Alaf au Ando ambazo kwasasa ndo kama fassion.,
Umetisha,
Hata ukubwa wa nyumba hujaufahamu/hajakupa umetaja bei. Unamaanisha nyumba yenye 100sqm itagharimu sawa na nyumba yenye 250sqm? Vipi kuhusu aina ya mabati anayotaka kutumia - bei yako inakuwa sawa kwa mabati ya aina zote?
Anyway: Mimi pia nipo nahitaji gharama za kuezeka nyumba iliyopo Makongo (DSM) yenye sqm 200. siyo ya ghorofa, bati za wanazotengeneza ALAF (za rangi).
Mkuu nyumba ikipauliwa vibaya hata iwe imejengwa vizuri namna gani na kufanyiwa finishing nzuri namna gani itachukiza kwenye macho ya watu tu. 3m ni gharama ya kawaida kabisa,Mkuu ufundi wa kuezeka tu mil 3? @zembemkuu
Mkuu ufundi wa kuezeka tu mil 3? @zembemkuu
nyumba ina ukubwa gani? hata hivyo andaa fedha za mbao treated timber kama 3.5m na bati 5m na ufundi 3m, kama hujapata fundi ni PM nije nicheki site then tutaongea.
Mie nguvu zikaniishia kabisa maana ndo nitakaribia stage hizo sasa huku sikutishana uku.Nilifikiri nimestuka peke yangu
Mkuu ufundi wa kuezeka tu mil 3? @zembemkuu
Usiogope maana hata majibu yenyewe hayaja dadavua vizuri, mfano hizo bati za kisasa lazima ujue vipimo halisi na aina la paa sasa hapo sijui ametumia vipimo gani, pia ikijulikana aina ya paa itasadia kujua mbao kiasi gani na za size ganimie nguvu zikaniishia kabisa maana ndo nitakaribia stage hizo sasa huku sikutishana uku.
Hata ingekuwa hela sio ngumu, ila kwenye ile hela imeandikwa hela halali na ni kwa malipo halali, inabidi kujua bei halali ili malipo halali yafanyike kwa kutumia hela halaliAsante Dancani maana hela ngumu hii, taarifa za wadau wengine wenyw uzoefu ni muhimu
Huyu fundi majanga. Kwa hesabu yake hata ukichukua utaratibu wa kutoa asilimia inayotokana na gharama za vifaa ndio iwe charge ya fundi haiwezi fika huko.
Kama anatumia mabati ya IT 5 na mbao za treated hiyo gharama ta ufundi inaweza kuzidi.
Mkuu unakubaliana na hizi gharama?
Mkuu ufundi wa kuezeka tu mil 3? @zembemkuu
Mkuu kupaua gharama ndiyo maana nyumba nyingi zinakwama kwenye linta.