Mfua suleiman
Member
- Feb 27, 2014
- 60
- 62
JITIHADA ZA HARAKA ZINAHITAJIKA:
Hili la kupanda kwa bei ya chakula nchini si jambo la kulifanyia masihara hata kidogo ikiwa tuna dhamira nzuri na watu wetu ambao walituamini na kutufanya tuendelee kua chama tawala katika taifa letu (Tanzania)
Nashangazwa sana na uwezo wa kufikiri wa vijana wenzangu wa CCM kwa namna wanavyoshindwa kua wakweli katika mambo kadha wa kadha yanayotokea katika nchi yetu.
Kuna mambo mengi sana ikiwemo swala la kupanda kwa gharama za maisha inayopelekea pia bei ya bidhaa muhimu kupanda, hii ikihusisha pia Chakula.
Haya na mengineyo ndio tunapaswa kuwashauli viongozi wetu ili wajue namna gani nzuri ya kupunguza ukali wa maisha ya watu wanaotufanya tutembee kifua mbele huku tukiendelea kupata heshma ya kua chama tawala nchini lakini pia kua moja ya chama cha siasa kikongwe katika bara la Africa na Dunia.
Inashangaza kuona vijana wenzangu wa ccm wakiwa bize kwenye mitandao kupost habari za Mbowe (KUB) kuwakimbia polisi....!! mara sijua kaenda kubadilisha damu...!! Mara sijui Tundu Lissu hafai kua rais wa TLS..... n.k
Sasa habari hizi zinamsaidiaje mwananchi wa wa kawaida ambaye anakula mlo mmoja asioshiba kwa siku!!?? Lakini pia alikua akinunua kilo ya sembe kwa kwa tsh 900/= mpaka 1200/= miezi minne iliyopita! lakini sasa ananunua kwa Tsh 1800/= mpaka 2100/=.
Chonde chonde vijana wenzangu wa ccm dhamira zetu za kutaka U-DC na nafasi zengine za uteuzi zisitufanye tuupindishe ukweli kwa kuubatiza jina la Plopaganda za Ukawa.
Lazima ifike mahali tujitambue kua sisi ni vijana wa Chama kilicho katika hatamu ya uongozi wa taifa letu hivyo tuna kila sababu ya kukosoa,kusimamia na kushauli viongozi wa chama na serekali wanaotekeleza Ilani ya Chama.
Kwa unafiki wetu wa kusifia kila jambo linalofanywa na viongozi wetu hata kama ni la Hovyo basi yatupasa kutambua kua hatulisaidii taifa, Chama na viongozi wake bali tunashiriki kufanya mambo yasiende viuri huku mitaani kwa walala hoi wenzetu kwa kua hatuthubutu kuwaeleza viongozi wetu Wasikivu ukweli tunaoujua kuhusu hali za maisha ya wanaotufanya tutembee kifua mbele.
Pamoja na hayo vijana wenzangu wa Ccm hatupaswi kutumia muda mwingi kulumbana na vijana wenzetu wa Chadema,Cuf, Act na vyama vigine vya upinzani.
Yatupasa kujua kua vijana hao wa upinzani wanatimiza wajibu wao kukosoa Chama tawala kwa kua dhamira ya vyama vyao ni kushika hatamu ya uongozi wa nchi.
Jukumu letu kubwa ni kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) viongozi wake na Serekali kwa ujumla kuhakikisha tunatekeleza Ilani yetu ya uchaguzi kwa vitendo ikiwemo kua na Tanzania ya viwanda kama tulivyoahidi kwenye Kampeni. "Nawasilisha"
Mfua S.L
Mvomero-Morogoro