Kuolewa SIO bahati...USIBAHATISHE!

Hua nashangazwa sana na kauli isemayo "kuolewa ni bahati" toka kwa wanaume na hata wanawake. Kauli hii hua inatoka kwa watu wanaoamini kwamba kwa kuolewa, mwanamke anakua amefanyiwa FAVOUR, AMESAIDIWA au AMEPEWA ZAWADI kana kwamba mwanamke pekee ndie anaefaidika na hiyo ndoa. Na hiyo bahati yenyewe inayotokana na kuolewa huko sio kupata mume ambae anastahili kuitwa mume bali ni kupata mahali pa kulala, chakula na mavazi. Wengine hua wanafika mbali kiasi cha kuwauliza wenzi wao moja kwa moja "unalalamika nini wakati unakula, unalala na unavaa vizuri?" pale mwanamke anapoonyesha kutoridhisha na namna mahusiano yao ndani ndoa yanavyoenda mf. mume kutokua mwaminifu, kutokuwepo nyumbani muda wa kutosha, kulewa sana, kumdharau mkewe n.k .

Ina maana wanawake wanaolewa ili wale, walale na wavae? Walipokua kwa wazazi wao au wakijitegemea waliishi bila kula, kuvaa na kulala ndani ya nyumba?

Kinachonisikitisha ni kuwa baadhi ya wanawake wanaunga mkono mawazo haya. Wanakubali kuchukuliwa kama watu wanaopewa msaada kwa kuolewa.

Binafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati". Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.

Kuoa/kuolewa sio bahati hivyo usibahatishe.
Ni kweli kabisa jamii kwa sehemu kubwa wanaamini kuolewa ni bahati,haijarishi unaeolewa nae, binafsi huwa nashangaa maana siamini kama kuolewa ni bahati, kwa imani hizo ndo maana wanawake wengi wananyanyasika kwenye ndoa zao.
 
Ukitaka kujua kama ni bahata au la jaribu kuongea na wadada wenye umri zaidi ya 35 utasikia malalamiko yao, kuna dada jirani amejaribu mpaka kuokoka ili apate mme lakini la kwa sasa mwenyewe anasema hana bahati.
 
...madhali mwanaume ndiye anayetamka "nakuoa!..."
kuolewa itaendelea kuwa bahati.
Mbu watu wanapokula kiapo cha ndoa kila mmoja anaulizwa kama "anakubali kumchukua mwenzake" na hamna anaeulizwa kama "anakubali kuchukuliwa na mwenzake". . .
 
Back
Top Bottom