Kuolewa si bahati, bahati ni kupata mume - a real husband.
Namaanisha, unaweza kuolewa na king'asti, play boy, mlevi, teja, abuser...
Kazi kweli kweli.KBinafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati".Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake.
Binafsi siamini wala sioni ni kwa namna gani "kuolewa ni bahati". Kwangu mimi bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake, anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake, anaemsikiliza mwenzake, anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . . wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu.
Kuoa/kuolewa sio bahati hivyo usibahatishe.
Unasema kweli. Lakini tatizo la wanawake walio wengi hawataki kujishughulisha kama wanaume wanavyo jishughulisha.
Ndio maana watu kama hao huwa wanauza miili yao. na wakipata mwanaume japo wa kuwafanya wale WANAONA BAHATI.
Lakini kwa mwanamke mwenye fikra komavu hawezi kuona kuwa kuolewa ni bahati.
Jaribu kuwa muelewa, nilichosema ni kwamba kitendo cha kuolewa tu pekee(na mtu yeyote yule) sio bahati, bahati ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa maana ya mahusiano yake (mwenye heshima, kujali, mwaminifu n.k).Kazi kweli kweli.
Mtoa mada anasema; Kuolewa haoni kama ni bahati, afu pale pale anasema bahati ipo kama umepata mtu ambae anaelewa nini mana ya ndoa.
Freeman,
Mwanaume anaweza akawa yeyote kati ya uliowataja lakini akawa anakupenda kwa dhati.
Hao watakuwa watoto wa mama!!!Na wanaume wanaosema hivyo je?
nikweli usemayo,lakini tatizo la vijana wengi wasasa hawaangalii sifa za msingi pindi wanapotafuta mwenzi pamoja nakwamba c bahati lakini na hayo yanachangia kwa ndoa nyingi kutodumu.
with a gud husby una the greatest bahati