Ibrahim Nzunda
Member
- Dec 7, 2012
- 23
- 22
WanaJF habari...
​
Kama mwanaume akimwambia mwanamke akisema Unajua mimi nakupenda sana tena nakupenda saana Lakini sipo tayari kua bwana wako. Yaani sipo tayari kua mume wako. Je, mtu huyo atakua anampenda kweli huyo mwanamke? Basi maana ya kuokoka inapatikana kwenye huu mfano. Kwa maana wengi wanamwamini Yesu kua ndie Mwokozi wao lakini hawataki kumkiri na kumkubari awe Bwana wao (uvuguvugu).
Ni sawa na kumwita mchumba wako "mke wangu" au "mume wangu" lakini hutaki kwenda kujiapiza mbele za Mungu na watu wake (i.e mchungaji/) kwamba "NDIYO NA KUBARI" (YES I DO). Watu kama hawa wanaambatana na matendo ya mwili ambayo dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. (wagalatia.5:19-21)
Kwamfano; kuna watu wengi sana wanashudia kuwa "Yesu ni Bwana" lakini kwa miaka yote hiyo hawajawahi sema hivya kwa Yesu mwenyewe kuwa "wewe Yesu ni Bwana wangu". kwahiyo wanashuhudia kwa watu na tena wanaimba kabisa makanisani kuwa Yesu ni Bwana wao lakini kwa muda wote huo hawajawahi hata siku moja kumwambia Yesu kua "kweli wewe Yesu ni Bwana wangu".
Anaekiri kwa Yesu kuwa "Wewe Yesu ni Bwana wangu" ndie alieokoka. lakini yeye anayeshuhudia kwetu tuu na kutuambia sisi kuwa Yesu ni Bwana wake lakini hajamwambia Yesu hayo maneno anayotuambia sisi huyo bado hajaokoka. kwa maana bado hajajiapiza kwa Yesu na kukubali awe Bwana wake.
Kuokoka ni kitendo cha wewe kukubali kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kwa kumkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako kua Bwana na Mwokozi wako, na hivyo unakua umetahiriwa kiroho na kuzaliwa upya (born again) kwa njia ya rohoni (warumi 2:28-29, 10:10,1petro 1:23).
Kuokoka sii kwa dhehebu flani tuu, bali ni kwa wote na madhehebu yote. Lakini wengi sana ni wapagani, kwani Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. Kuokoka ni kukubali kua mkristo. Mkristo maana yake ni mtu wa Kristo yaani yule ambae Yesu ni Bwana na Mwokozi wake.
Kwahiyo nikisema mimi nimeokoka, vilevile ninakua namaanisha kwamba hapa duniani nimeokolewa kutoka katika utawala wa shetani/giza na kupewa utawala wa Mungu kwa kupewa Roho Mtakatifu, ambaye ndiye guarantee ya uzima wa milele (waefeso.1:13-14).
Hivyo Kuokoka pia ni utimilifu wa imani yako kwa kupokea wokovu kwa kumuamini Bwana Yesu, kwani maana ya imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni udhahiri wa mambo yasiyoonekana (Waebrania.11:1)
Kuokoka ni kitendo cha wewe ku-sign kua mwana wa Mungu kwa kukubali kuwa mtakatifu kwa utakaso wa damu ya Yesu na Hivyo wewe kupewa Roho Mtakatifu ambae kwa huyu unapigwa mhuri katika roho yako kama garantii ya wewe kuepuka/kuokolewa na adhabu ya mauti ya milele ndani ya ziwa la moto wa milele. Kwamaana bila ya utakatifu, hakuna atakae mwona Bwana. (Waebrania 10:10, 12:14 Waefeso 1:13-14 na Wagalatia 3:26-29)
Vile vile kwa mdomo Adam alidanganywa na hatimae vizazi vyote vikapata mauti. Basi tena kwa mdomo wako unapata wokovu pia. Yaani kama vile kosa la mtu mmoja (Adam) lilivyoleta hukumu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la mtu mmoja (Yesu) la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima kwa wote (Warumi.5:12-19, 10:8-13)
Neno Bwana maana yake ni Lord ambayo pia ni Owner. Kwa hiyo ukisema Yesu ni Bwana wangu inamaana Mungu anakumiliki, roho yako imezaliwa upya (born again), na mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu na wala sio wako tena. Kwahiyo lazima awe Bwana, kwani Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa (1wakorintho.6:13-20, Yakobo 2:26)
Kuongoka ni neno linalotoka na ongoa na maana yake ni convert. Lakini neno kuokoka (to be saved) ni kitenzi cha nomino wokovu ambayo ni salvation. (math:18:3,Maten.15:3-11,1tim.3:6)

MSINGI NA MAANA YA KUOKOKA
Ndugu zangu
bila kuficha imeandikwa kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini na hivyo kuhesabiwa haki, tena kwa kinywa mtu hukiri na hivyo kupata wokovu. Na chini kidogo inasema Kwa maana, Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka na tena imefafanuliwa waziwazi kabisa kua Tazama, wakati uliokubalika ndio huu. Tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa. Kwani baada ya Kristo, mwandamu amewekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu. (Warumi.10:8-13, 2wakorintho.6:1, waebrania.9:27)
Kuokoka ni kitendo cha wewe kukubali kubatizwa kwa Roho Mtakatifu kwa kumkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako kua Bwana na Mwokozi wako, na hivyo unakua umetahiriwa kiroho na kuzaliwa upya (born again) kwa njia ya rohoni (warumi 2:28-29, 10:10,1petro 1:23).
Kuokoka sii kwa dhehebu flani tuu, bali ni kwa wote na madhehebu yote. Lakini wengi sana ni wapagani, kwani Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. Kuokoka ni kukubali kua mkristo. Mkristo maana yake ni mtu wa Kristo yaani yule ambae Yesu ni Bwana na Mwokozi wake.
Kwahiyo nikisema mimi nimeokoka, vilevile ninakua namaanisha kwamba hapa duniani nimeokolewa kutoka katika utawala wa shetani/giza na kupewa utawala wa Mungu kwa kupewa Roho Mtakatifu, ambaye ndiye guarantee ya uzima wa milele (waefeso.1:13-14).
Hivyo Kuokoka pia ni utimilifu wa imani yako kwa kupokea wokovu kwa kumuamini Bwana Yesu, kwani maana ya imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni udhahiri wa mambo yasiyoonekana (Waebrania.11:1)
Kuokoka ni kitendo cha wewe ku-sign kua mwana wa Mungu kwa kukubali kuwa mtakatifu kwa utakaso wa damu ya Yesu na Hivyo wewe kupewa Roho Mtakatifu ambae kwa huyu unapigwa mhuri katika roho yako kama garantii ya wewe kuepuka/kuokolewa na adhabu ya mauti ya milele ndani ya ziwa la moto wa milele. Kwamaana bila ya utakatifu, hakuna atakae mwona Bwana. (Waebrania 10:10, 12:14 Waefeso 1:13-14 na Wagalatia 3:26-29)
KWA KINYWA CHAKO UNABATIZWA KWA ROHO MTAKATIFU
Kutumia mdomo ni muhimu kabisa kwasababu kuna sheria iliwekwa na Mungu kua Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi. Kwahiyo kwa ulimi wako mwenyewe utapata uzima wa milele kwa kukikiri kwa kiny​wa chako kwamba Yesu ni Bwana. Vivyo hivyo, kwa kinywa chako unaweza kupata mauti ya milele kwa kumkana Kristo au kwa kiburi cha wewe kuto kukiri kua Yesu ni Bwana wakati ukiwa hai hapa duniani. (Mithali.18:21).
Vile vile kwa mdomo Adam alidanganywa na hatimae vizazi vyote vikapata mauti. Basi tena kwa mdomo wako unapata wokovu pia. Yaani kama vile kosa la mtu mmoja (Adam) lilivyoleta hukumu kwa watu wote, vivyo hivyo pia kwa tendo la mtu mmoja (Yesu) la haki huleta kuhesabiwa haki kule kuletako uzima kwa wote (Warumi.5:12-19, 10:8-13)
UKISEMA YESU NI BWANA LAZIMA UWE NA DHAMIRA YA KWELI
Wengi wanasema na tena wanaimba kila siku makanisani mwao kua Yesu ni Bwana lakini hawajatia nia mioyoni mwao. Na kwa watu kama hawa Mungu anasema Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Huniabudu bure.(Marko.7:6-7).
Neno Bwana maana yake ni Lord ambayo pia ni Owner. Kwa hiyo ukisema Yesu ni Bwana wangu inamaana Mungu anakumiliki, roho yako imezaliwa upya (born again), na mwili wako ni hekalu la Roho Mtakatifu na wala sio wako tena. Kwahiyo lazima awe Bwana, kwani Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa (1wakorintho.6:13-20, Yakobo 2:26)
KUONGOKA VS KUOKOKA
Kuongoka maana yake ni kusilimu. Ni kubadilisha mfumo/imani moja kwenda nyingine. Kwa mfano Mtume Paulo aliongoka kutoka dini ya kiyahudi na baadae kuokoka kwa kupewa Roho Mtakatifu. Lakini wanafunzi 11 wa Yesu wao hawakuongoka bali waliokoka kwa kujazwa na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo mtu anaezaliwa kwenye familia ya kikristo yeye haongoki bali anachohitaji ni kuokoka.