Kuoa mke wa pili raha sana sana, heshima katika ndoa inaongezeka sana

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
17,667
18,973
MMU habari zenu,

Kwa wale ambao wako katika ndoa watanielewa haraka, na sitaki kumkwaza mtu kwa sababu za dini au imani yake.Ukiwa katika ndoa ya mke wa kwanza, kuna changamoto nyingi na kama mwanaume rijali, inabidi utimize mahitaji yote ya msingi na ya ziada katika ndoa na familia.

Sasa ukija kuoa mke wa pili, yaani una wake wawili, ndoa inakuwa tamu sana na heshima inaongezeka sana katika ndoa, kila mke anajitahidi sana sana kuwa makini na mahaba yanakuwa kumzidi mwenziwe hawasemi, ila kama mwanaume utaona mabadiliko kuliko wakati ukiwa na mke mmoja.

Kuanzia mapishi, usafi, kukujali, mahaba yanaongezeka, na hadi mavazi kila mke anavaa vema zaidi kuliko wakati akiwa mke mmoja pekee.Mwanaume utaona utamu sana, yaani ukifika home tu kwa mke yeyote, utaona mautamu tofauti na awali naona sababu labda kila mke anajua sasa ni mashindano, hawasemi, ila utaona mapenzi matamu matamu. Kweli kuwa na wake wawili halali ni tamu sana.

Karibu mke wa pili, dunia ni yako, mko wawili sasa, acheni wivu, mpendane na nitawalea kama malkia milele kwa mapenzi tele tele. Ndoa
ya wake wawili tamu sana sana.
 
Dunia ina maonevu kweli maana kwa mdogo wangu hali haipo hivyo akiuliza hata kitu kidogo kwa mke huyu anaambiwa kwani huyo mkeo hakufanyii!
Akiuliza chakula kule nako anaambiwa kale kwa huyo mkeo, kwa ujumla amekonda kama kaoa dunia maana kila mwanamke ana donge moyoni kwa kudhani yeye hapendwi ila mwenzake ndio anaependwa na hata akipeleka vitu sawa lakini bado ataambiwa huko itakuwa umezidisha.

Sasa hapo rabda aongeze wawili wengine tuone itakuwaje
 
unafurahi maana unategea kutunza familia zite mbili unalelewa! nani asiyejua maswaibu wayapatayo wake wenza maana kwakuwa wanashindana hela ya matumizi hutoi

No problem with monies.. fedha ipo ya kutosha na kusaza, ya kila mmoja kuwa na luxury home, car and sweet account.. am talking MAPENZI yalivyo kuwa matamu sbb kila mmoja anachangamka kimahaba kweli kweli...!!
 
Dunia ina maonevu kweli maana kwa mdogo wangu hali haipo hivyo akiuliza hata kitu kidogo kwa mke huyu anaambiwa kwani huyo mkeo hakufanyii!
Akiuliza chakula kule nako anaambiwa kale kwa huyo mkeo, kwa ujumla amekonda kama kaoa dunia maana kila mwanamke ana donge moyoni kwa kudhani yeye hapendwi ila mwenzake ndio anaependwa na hata akipeleka vitu sawa lakini bado ataambiwa huko itakuwa umezidisha.

Sasa hapo rabda aongeze wawili wengine tuone itakuwaje

Ni kweli usemayo..ila kama huna FEDHA za kutosha, USIOE MKE WA PILI...usijaribu
 
No problem with monies.. fedha ipo ya kutosha na kusaza, ya kila mmoja kuwa na luxury home, car and sweet account.. am talking MAPENZI yalivyo kuwa matamu sbb kila mmoja anachangamka kimahaba kweli kweli...!!
Sasa kama unazungumzia life hiyo sio tu wanawake wawili, hata uweke wanawake hamsini watatulia tu kwa sababu ac imenona
 
hapo tafuta na mchepuko ili wawe wanapigiana simu wanaulizana leo upo wapi
 
Sasa kama unazungumzia life hiyo sio tu wanawake wawili, hata uweke wanawake hamsini watatulia tu kwa sababu ac imenona

Hapana, wawili mwisho... sbb wakiwa zaidi ya hapo haifai, wake wawili ndio naweza gawa love and wealth fairly, wakiwa watatu ni ngumu kidogo..!!

Hata kugawa mapenzi kuanzia wake 3 ni ngumu kidogo, hata kama una fedha za kutosha mno kuwatunza na kuwapa luxury life...!! Wawili hapo mwisho.. hakuna cha mchepuko wala nn...!! Unajua kuna wanaume wengine wanakwambia wana mke mmoja, BUT BEHIND THE DOORS ana michepuko kama 5 hv.. hiyo ndio mbaya sana
 
MMU habari zenu,

Kwa wale ambao wako katika ndoa watanielewa haraka, na sitaki kumkwaza mtu kwa sababu za dini au imani yake.Ukiwa katika ndoa ya mke wa kwanza, kuna changamoto nyingi na kama mwanaume rijali, inabidi utimize mahitaji yote ya msingi na ya ziada katika ndoa na familia.

Sasa ukija kuoa mke wa pili, yaani una wake wawili, ndoa inakuwa tamu sana na heshima inaongezeka sana katika ndoa, kila mke anajitahidi sana sana kuwa makini na mahaba yanakuwa kumzidi mwenziwe hawasemi, ila kama mwanaume utaona mabadiliko kuliko wakati ukiwa na mke mmoja.

Kuanzia mapishi, usafi, kukujali, mahaba yanaongezeka, na hadi mavazi kila mke anavaa vema zaidi kuliko wakati akiwa mke mmoja pekee.Mwanaume utaona utamu sana, yaani ukifika home tu kwa mke yeyote, utaona mautamu tofauti na awali naona sababu labda kila mke anajua sasa ni mashindano, hawasemi, ila utaona mapenzi matamu matamu. Kweli kuwa na wake wawili halali ni tamu sana.

Karibu mke wa pili, dunia ni yako, mko wawili sasa, acheni wivu, mpendane na nitawalea kama malkia milele kwa mapenzi tele tele. Ndoa
ya wake wawili tamu sana sana.

Ujagundua umewapa mwanya wa kuendelea na wapenzi wa nje, maana kukosa heshima usababishwa na kushindwa kukabili majukumu pia. Wanawake sio housemaids
 
MMU habari zenu,

Kwa wale ambao wako katika ndoa watanielewa haraka, na sitaki kumkwaza mtu kwa sababu za dini au imani yake.Ukiwa katika ndoa ya mke wa kwanza, kuna changamoto nyingi na kama mwanaume rijali, inabidi utimize mahitaji yote ya msingi na ya ziada katika ndoa na familia.

Sasa ukija kuoa mke wa pili, yaani una wake wawili, ndoa inakuwa tamu sana na heshima inaongezeka sana katika ndoa, kila mke anajitahidi sana sana kuwa makini na mahaba yanakuwa kumzidi mwenziwe hawasemi, ila kama mwanaume utaona mabadiliko kuliko wakati ukiwa na mke mmoja.

Kuanzia mapishi, usafi, kukujali, mahaba yanaongezeka, na hadi mavazi kila mke anavaa vema zaidi kuliko wakati akiwa mke mmoja pekee.Mwanaume utaona utamu sana, yaani ukifika home tu kwa mke yeyote, utaona mautamu tofauti na awali naona sababu labda kila mke anajua sasa ni mashindano, hawasemi, ila utaona mapenzi matamu matamu. Kweli kuwa na wake wawili halali ni tamu sana.

Karibu mke wa pili, dunia ni yako, mko wawili sasa, acheni wivu, mpendane na nitawalea kama malkia milele kwa mapenzi tele tele. Ndoa
ya wake wawili tamu sana sana.
Tamaa ilimponza fisi
 
hongera zako wewe uliye na wake wawili na unaenjoy maisha maana huku wenzako mke mmoja michepuko sita na wote wanapata huduma na tunaishi maisha ya mashaka sana na simu zetu tuwapo nyumbani sasa sijui hata kunachotushinda kuungana na wewe ni nini..aibu juu yetu..,
 
Back
Top Bottom