Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79

Wakuu,

Kunuka harufu mbaya (kikwapa) ni ugonjwa au uchafu? kama ni ugonjwa kuna dawa?

Kuna hii hali ambayo mtu ananuka kikwapa wakati wa kula tunda (wakati mwingine aaaah yuko safiii tu). Je, inatokana na nini? Na nini kifanyike ili kuzuia hali hiyo?


MASWALI NA MAHITAJI YA WADAU WENGINE
Jamani naomba msaada kwenu kwa anayeifahamu dawa ya kumaliza tatizo hili kwa sababu ninaye mtoto wa miaka 11 wa kike anasumbuliwa na tatizo hili (la kunuka kwapa) hata atoke bafuni kuoga au ni ugonjwa wa kurithi?
Watalaam,

Naomba kujuzwa dawa ya kutumia ili kuondoa harufu ya kikwapa.

Asante.


MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU
Jambo hilo huwakwaza watu wengi na hivyo kujikuta wakitengwa bila kujua sababu.

Kunuka kikwapa ni tatizo kubwa katika mwili wa binadamu. Tatizo hili husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu chini ya kwapa.

Sasa basi, kuna njia nyingi ambazo watu wengi huzitumia ili kwapa liwe na harufu nzuri, kavu na safi.

Wengine hutumia njia za kisasa ambazo ni pamoja na kupaka doodoranti au pafyumu zinazosaidia kuondoa harufu mbaya mwilini.

Lakini kama hiyo haitoshi, kuna njia za kisasa zinazoweza kuzuia harufu ya kwapa ambazo ni pamoja na kupaka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya.

Kuvaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufi zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kuwa kavu, safi na bila harufu mbaya.

Kuoga kila siku na kusafisha nguo kwa maji safi kunasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya.

Pia kunywa maji mengi kila siku kunakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.

Njia nyingine inayoshauriwa ni kuhakikisha kuwa unaosha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps).

Aidha, kupunguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguu. Inasemekana kuwa kula vitunguu vingi kunachangia mwili kutoa harufu kali.

Licha ya pafyumu na spray kusaidia kuondoa harufu mbaya mwilini, hii si dawa endelevu kwani baada ya muda harufu inaweza kurudi palepale hivyo ni vema kutumia njia za asili kukabiliana na hali hiyo. Pafyumu haiwezi kutibu tatizo moja kwa moja.

Pia inashauriwa kuwa baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao huwavutia bakteria kukua katika maeneo yaliyojificha (yenye mikunjo).

Mbinu nyingine ni kujitahidi kunyoa nywele za kwapa mara kwa mara na kuepuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.



ZAIDI, SOMA:

Kunuka kikwapa ni nini?

Hii ni harufu kali inayotoka kwenye sehemu ya juu kabisa ya mkono kwa chini au kwa jina la kikwapa.

Chanzo ni nini?
kimsingi harufu hii hutokana na bacteria kutumia jasho la binadamu na kutengeneza aina fulani ya tindikali ambayo hutoa harufu. Katika hali ya kawaida jasho binadamu hua halina harufu mpaka pale linapokutana na bacteria ambao hushambualia jasho lako. Mara nyingi binadamu huanza kutoka harufu sana akibalehe au kuvunja ungo ambapo manyoya huanza kuota kwenye kikwapa lakini pia watu wanene sana, wanaokula vyakula vyenye viungo vingi na wenye baadhi ya magonjwa kama kisukari.

Harufu kwenye mwili wa binadamu ukiachana na makwapa pia hutoka sehemu za siri, miguuni, kwenye mikunjo ya nyama kwa wanene, nyuma ya masikio, sehemu ya haja kubwa, katikati ya mapaja, na kwenye nywele za sehemu za siri. Apocrine gland ni sehemu ya mwili ambayo inatengeneza jasho, huapatikana sehemu mbalimbali za mwili kama kwapa, ngozi, matiti,na kadhalika.

Jinsi ya kuzuia harufu
  • Weka safi kwapa lako kwa kuosha na maji safi na sabuni ya kuua bacteria.
  • Tumia deodorant na body spray, mara nyingi hupunguza wingi wa jasho na kukupa harufu nzuri
  • Oga kila siku angalau mara mbili asubuhi na jioni kwa maji ya moto kwani maji ya moto yanasaidia sana kuu bacteria walioko kwenye ngozi.
  • Vaa nguo nyepesi ambazo zinakupa nafasi ya mwili kukausha joto kwa upepo, hivyo usivae nguo nzito sana.
  • Usile vyakula vyenye viungo vingi sana kama kitunguu swaumu lakini pia utafiti umeonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu huweza kuongezea harufu ya mwili.
  • Kunywa maji mengi sana kwani yanasaidia kusafisha mwili wako.
  • Nyoa manyoya ya kwapani kila yakiota kwani ni kihifadhi cha harufu kali.
Matibabu
  • Upasuaji; wakati mwingine upasuaji kitaalamu kama endoscopic thoracic sympathectomy ambayo hufunga mishipa ya fahamu ambayo hufanya jasho litoke jingi hufanyika kutibu tatizo hili..
  • Baadhi ya magonjwa ya figo, maini, fangasi, kufunga kwa hedhi kwa akina mama wa umri mkubwa huweza kusababisha hali hii hivyo muone daktari kwa vipimo zaidi na matibabu kama haupati nafuu.
Ni wakati gani unatakiwa umuone daktari?
  • Kutokwa na jasho sana wakati wa usiku.
  • Kutokwa jasho zaidi kuliko mwanzoni.
  • Jasho linaanza kukuzuia na kazi zako za kawaida.
  • Kutokwa na jasho sana wakati wa baridi.
  • Kuwashwa sana na ngozi.

Chanzo: sirizaafya.info
 
Naomba nikuambie hivi mwambie awe anasafisha maeneo yake mpka ndani kila akikoga na pia atumie fame wash kwa ajili ya kukata harufu na usafi pia. Zipo fame wash za oriflame, na nyingine nyingi tu.
 
sanaa mkuu hajui huyu!.
bytheway nimekugongea senksi, thibitisha hapahapa:

Nimekujibu mpwa! Kaangalie. Watu wengine bana! Eti wanaogopa harufu ya kikwapa wakati wenzao hata harufu ya ushuz.i mzito kwao burudani!
 
Pole journal!! kutoa harufu ya kikwapa huwa haina sababu maalum, inawezekana ikawa ni maumbile au ufanyaji wa kazi za kutumia nguvu na nk. Dawa yake niijuayo mimi ni deodorant!! but also kuna vitu kama sabuni ya omo.

Huyo anaetoa harufu awe anaosha kikwapa chake na omo kila mara anapopata nafasi. Au anaweza akapaka ndimu katika kikwapa huwa inakata harufu. Apake mara kwa mara anapopata muda, ataona matokeo yake.
 

Du! Huo utafiti ulifanywa na dr. gani? nipeni jina lake nimfute kazi. Unamshauri mwenzio apate cancer siyo?
 
Jamani hii harufu naipenda sana kuisikilizia, huwa sipendi kabisa kuona shemeji yenu anatumia deodrant, na mara nyingine huwa nazificha ili nipate kusikia hii harufu, sometime akilala huwa naweka pua yangu kwapani kwake nisikie vizuri harufu hii, nimekuwa kama teja.

Hivi hii kitu kuna wengine wenye kupenda?
 
Unajua kucheka nako kunasaidia ngoja niendelee kujichekea maana mkuu Bwabwa una mambo, kama jina lako lilivyo!Lol
 
Jicheki mzee, maana unaweza ukaanza kupenda harufu ya ****** halafu hasa vile vya stendi na sokoni.
 
I think you are in some kind of trouble. You should seek help.
 
Haya mambo ni mtu na mtu. mnaijua harufu ya watu wazima ambayo hata akioga bado unaisikia? nadhani ndiyo anayoiongelea.

Niliwahi kuwa na uhusiano na binti mmoja mwaka 96 alikuwa na harufu kali sana hata akioga namna gani haiishi hata akipiga pafyum, ukimkumbatia unaisikia. loh, nilitokea kuipenda sana ukichanganya na ujana wangu wakati ule ilikuwa inanipa wazimu kabisaa.
 

Mmmh, watch out!! Unaweza kuwa mjamzito, manake nilisikia waja wazito ndo huwa wanavutiwa na hizo harufu.
 
Kama harufu uipendayo ni ile kabla ya kutumia deodorant, inategemea kama ana mkwapa unatema ka viatu vya michezo na we unafurahia basi we mgonjwa. Lakini its good to be natural mwambie aoge mara kwa mara. Halafu we badala ya kumfurahisha mkeo kwa kumtimizia haki yake ya ndoa we unang'ang'ania kutia pua yako kubwa kama kiganja kwenye kwapa la mwenzio basi we mgonjwa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…