Kunguru kunidonyoa kichwani

Duh shukrani
 
Aisee
 
Huwa wakitoka hapo wanahamia kwenye majicho.

Anza kuvaa miwani kabla letina hazijanyofolewa.


Hahahaha

Ila usijali hatua za kwanza anza kutembea na kofia ya bodaboda
 
Muda sio mrefu utakua chizi huo ni uchawi wa kumfamya mtu achanganyikiwe wahi kanisani au kwa sangopa imani yako ilipo.
 
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi

Huo udalali wako unaofanya na kula hela za watu utakutokea hapo ulipodonolewa!
Kaombe msamaha wale jamaa wote uliokula hela zao, hao kunguru hawatakuacha...
 
Mbona sasa anaulizwa na hasemi ikiwa amewahi kuwakwaza hao ndege?

Jambo la kujua ni kwamba wanyama na ndege japo hawaongei lugha zetu lakini wana lugha zao na ishara zao wao wanaelewana. Pia wana tabia na matukio.

Kwa suala la kunguru, ndege huyo ana uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu za matukio. Na kwa mtu ambaye amewakwaza na hasa kwa kurudia rudia basi humkariri na kukabiliana naye.

Wanaweza kuwa wanakuja kwenye miti iliyo jirani au mahali unapoishi. Kama unawafukuza kwa kuwarushia mawe na hasa ukimdhuru mmoja wao, na hasa kama wana viota maeneo hayo basi ndugu wanaweza kukuaibisha ndege hao.

wanachofanya, kila wakikuona wanaanza kukuandama. Wanapishana kama wa akija kukubeba wanapita kichwani shaaaaa! Anarudi mwingine shaaaa! Unakwepa mpaka watu watajua wewe ndio wanakuhusu. Wanaweza kukufuata mpaka ofisini aisee.

Hakuna lolote baya kiimani lakini angalia namna ya kuepukana nao kwa kubadili njia ingawa akikuona mmoja tu unashangaa hawa hapa!

Sema sasa, unahisi sababu ni nini? Uliwakwaza?
 
Anza kutembea na vitu viwili hasa unapotoka nje, Sime yenye makali na element kama bodaboda kuna siku wataluja kwa wingi wakudonoe waondoke na ubongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…