Kunguru kunidonyoa kichwani

Mkuu nimecheka sana ila NIMEKUKUBALI.


Mtoa thread...............Ndoto zote zote unazosoma PLEASE piga goti omba majibu kwa MUNGU (Kama unaamini yupo) yeye ndio atakupa majibu sahihi ya ndoto yako.
 
KISWAHILI SAHIHI NI "KUDONOA" SIO "KUDONYOA".
 
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi
Pole ndugu! Kwanza si kawaida kwa kunguru kufanya hayo lakini pia si kwa mara moja tu umefanyiwa hilo. Maana ya kujirudia ni kuwa unahakikishiwa au unapewa msisitizo kuhusu hilo jambo kuwa hakuna utani.
Lakini kwenye neno la Mungu yapo majibu.
1. Kwanza kinachoshambuliwa ni fikra au fahamu zako. (Kwa sababu kilichoshambuliwa ni kichwa)
2. Pili ni adhabu kutoka na kosa ambalo mtu anakuwa amefanya. Ukitazama Kitabu cha Mithali 30:17 "Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling'oa, Na vifaranga vya tai watalila."

Kwenye neno "jicho" hapo juu weka neno "kichwa"

Kuna mama mmoja mwaka jana namaanisha 2020 alikuwa anasumbuliwa sana na ugonjwa fulani alipopelekwa hospitali ya kwanza Kunguru wakawa wanajazana juu ya lile jengo alimolazwa. Baadaye wakaona wamuhamishe wampeleke hospitali fulani ya Rufaa nako kunguru wakahamia juu ya jengo alikolazwa yule mama. Ndugu yake akawa anamsimulia hiyo habari muinjilisti mmoja ambaye ni mtumishi mwenzangu katika kituo ambacho nilikuwa nikifanyia kazi na ikawa ndiyo msaada kwao maana ndiye aliyewaongoza cha kufanya hata yule mgonjwa akapona.

HATUA ZA KUCHUKUA
Jitafakari ni wapi umemkosea Mungu kwa namna yoyote ile mfano
1. Umedhulumu mtu
2. Umemwibia mtu
3. Kama upo kwenye ndoa angalia mkeo au mumeo umemfanyia nini?
4. Watoto umewafanyia nini?
5. Nenda mbele zaidi kujitafakari mwenyewe ukimuomba Roho mtakatifu akukumbushe
6. Ukushajua makosa yako tubu na ugeuke(uache huo uovu)
7. Achilia damu ya Yesu Kristo kwenye mlango uliofunguka hata ukaletewa mashambulizi hayo ili ufungwe na usishambuliwe tena.
8. Omba Mungu kwa jina la Yesu Kristo akuondolee madhara ya mashambulizi uliyoyapata.
9. Omba Mungu akuongezee ulinzi wa kimbingu.
10. Acha kabisa uovu na umgeukie Mungu.
 
Una bifu na kunguru? maana kunguru wana visasi sana na hawawezi kusahau...........bora upige magoti umwombe msamaha kunguru.
 
Alidhani ni kunguru mwenzie πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi
 
Mkuu me nahisi kitu,
Unaweza kudhani unakichwa cha binadamu kumbe unatembea na dumple la takataka bila wewe kujua. Kwanini wewe tu? Mkuu huna kichwa cha binadamu. Me nahisi hivyo
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€
 
Habarini! hivi hili swala la kunguru kukudonyoa kichwani Lina maana gani? Mara ya kwanza kunitokea nikafikiri kwa vile nilivaa shati jeusi, lakini Leo pia imenitokea Cha kushangaza ni Mimi tu wengine hawadonyolewi
Uwe unaoga siyo kutembea na dampo kichwani.
 
Huwenda ulishawahi kumdhulumu mtu kwenye hizo inshu zako za udalali,huyo kunguru ni wa kamati maalumu
 
Nikiwa posta mwaka 2007 nadhurura zangu badae nikanunua simu NOKIA fulan hivi.. nikiwa nateembea karibia na DIT akaibuka kunguru from know where akaikwapua simu mpaka leo .... kunguru wa town ni shida sijui alijua nyama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…