Kunguru hafugiki

Kunguru hafugiki

Yeyote unayepitia uzi huu kama ni mwanaume usije ukafanya kosa la kumuoa bar maid.
Mwanamke akishakua baamedi huyo haoleki tena na hawezi kutulia na mume wako,
na km ukimuoa ukiigua au uchumi ukayumba lazima akukimbie
 
Wakuu mambo vipi!

Basi mwenzenu leo nimekumbuka nilivyoponzwa na yule muhenga aliyesema mapenzi ni maua popote huchanua.

Nilikua mteja mzuri sana wa bar moja huko songea maeneo ya msamala.Na hapo ndio nikajikuta katika kitanzi cha penzi la bar maid.Nilianza vizuri tu kwa kumuapproch kama wanawake wengine ivyo akaniona wa pekee sana maana wengine wote hua wanaulizia bei ya k.kitu kingine ni zile chenji zangu ambazo hua namuachia ndio zikafanya shughuli isiwe ngumu sana.Basi tukaelewana na baada ya kudumunaye kama miezi miwili nikajihisi tayari nimembadili na ninauwezo wa kumbadili zaidi awe mama bora chini ya himaya yangu.Nikamvuta getto,nikamuachisha kazi ya bar na nikamfungulia bucha ya kuuza samaki wakati mipango mingine ikiendelea.Alifanya vizuri katika biashara hiyo, baada ya miezi mitatu nikaona haina haja ya kumsimamia ivyo nimuache ajiendeleze mwenyewe.

Nilipata safari ya kwenda china(kufunga mzigo katika biashara zangu), cha ajabu nikakuta yule mbuzimawe kauza kila kitu kuanzia getto,akaenda dukani kwangu kadanganya nimemuagiza sh 4m. Na vijana wangu wa kazi walivyokua mbulula hata hawakunipigia simu kuniuliza kabla ya kumpa eti kisa wanajua ni mke wangu, hadi bucha ya samaki kabeba kila kitu na haijulikani alipoelekea.Kiukweli alinirudisha nyuma mno lakini kama mwanaume Nikajipanga upya na maisha yakaendelea.

Baada ya miaka kadhaa kupita nimekuja kumkuta bar fulani hapa dar es salaam anahudumia na usiku anauza k.Inasemekana pesa zote zile alikula bata na hakuna alichofanya.Hadi muda huu bado hajaniona wala hajajua kama nafahamu sehemu anapopatikana.Nimfanyaje mtu kama huyu?
HUWEZI MUACHA HIVI HIVI...AJUE TU KUWA UNAJUA NYUPO NA UNAMUONAGA...AU ACHA HATA MSG NOTE UMWAMBIE AM COMING FOR YOU NOW....
 
Back
Top Bottom