KUNENA KWA LUGHA

Herbert Nkuluzi

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
2,503
2,525
Mpendwa , somo la kunena kwa lughs ni somo pana kabisa kuliko wengi wamevyolichukulia lakini nina machache tu

1 Hoja yako ya kwanza umesema kuna baadhi ya mahubiri ya lugha za kigeni (kiingereza ) umemwona mkalimani anafasiri hadi nyakati za mhubiri kunena kwa lugha.
Kiuhalisia ni kwamba sio rahisi mtu kufasiri maneno ya watu wanaodai wananena kwa lugha kwa kuwa wanajaribu tu kudanganya tu watu ili waonekane wana Roho wa Mungu.Ni kweli Roho wa Mungu aliahidiwa kuwa atawawezesha watu kunena kwa lugha lakini ahadi hiyo inaonekana kutimia kwa kusudi fulani na ahadi yenyese haina mipaka ya ama ni daima au ni kwa muda fulani.Ungana nami kutazama hilo

Yesu anasema hivi

Marko 16:
17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;

Ukilitazama andiko hilo utaelewa kuwa kunena kwa lugha ni ahadi ya wale watakaoiamini Injili na ikumbukwe moja ya watu walioamini ni Mitume wa Yesu sasa tazama ahadi ilivyotimia kwao

Matendo ya Mitume 2:
1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Hapo tunaambiwa Roho aliwajalia kusema kwa lugha nyingine ambazo hata hivyo zilieleweka kwa wale waliokuwa wakizisikia yaani haikuwa just mlipuko wa ovyo wa kuongea bali watu walielewa kilichotamkwa pale soma
watu walivyoshangaa hilo

Matendo Ya Mitume 2:

6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe.

7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya?

8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo?


Maana yake ni kwamba tukio lile lililenga kuwaonesha watu uweza wa Mungu wa Israeli na zaidi kuwavuta watu kumwamini Mungu wa waisraeli na zaidi kumwamini Yesu mwenyewe kwa ahadi iliyotimia.Hivyo ni ukweli usiopingika kwamba kunena kwa lugha ilikuwa ni jambo la maana kubwa kuipeleka Injili mbali kabisa hasa kwa wapagani wa mataifa ya Arabuni na mashariki ya mbali ambao wanatajwa kuwapo Yerusalemu siku ile.Lakini Mungu hakaririki katika taratibu zake hivyo suala hilo lilipanuka kuwa katika namna nyingine baadae ndiyo maana tunaona mwendelezo ukibadilika kama alivyoelekeza Mtume Paulo hapa

1 Wakorintho 14:
2 Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake.

13 Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kufasiri.

Aya hii ya 13 inasema wazi ukitaka kunena kwa lugha sharti uombe ujue kile unachokinena , anaendelea

14 Maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.

Hapa tunaambiwa lugha hizo maalumu kwa wale wasiomini(huu ni mtazamo sawa na ule wa Matendo 2 )

22 Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio, bali kwao wasioamini lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.

23 Haya! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, je! Hawatasema ya kwamba mna wazimu?


Paulo anasema kama watu watanena tu bila kanuni hizo hapo juu watakuwa km wana wazimu.


24 Lakini wote wakihutubu, kisha akaingia mtu asiyeamini, au mjinga, abainishwa na wote, ahukumiwa na wote;

25 siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo atamwabudu Mungu, akianguka kifudifudi, na kukiri ya kuwa Mungu yu kati yenu bila shaka.

Anashauri wanenaji kwa lugha wawe si zaidi ya 3 na awepo mmoja wa kufasiri (Hapa inaonesha ni lugha tu za kawaida eg Kiingereza kwenda kiswahili )

27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.

28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.


Hapo anasema kama hakuna wa kufasiri basi anyamaze tu (Je, wakati wa Mitume kushukiwa na Roho Mtakatifu wafasiri walikuwepo? Jibu ni hapana

29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.


Ukitazama hapo juu utaelewa kwamba watu hawa wa sasa wanaongea tu lugha wasizozifahamu wala hata wale wanaowasikia hawaelewi chochote kabisa hivyo ni dhahiri unenaji wa sasa umepoteza kabisa ile mantiki iliyokusudiwa ya kunena kwa lugha yaani sio tu haina maana yoyote bali pia haina ukweli wowote.

Hebu jiulize
1.Kama kuna ukweli kwa nini wanene tu wakati wa kuomba?

2 Kwa nini hakuna ushahidi wa lugha zao kueleweka kwa watu wanaowasikia wakati wakinena km ilivyokuwa kwa Mitume siku ya Pentekoste?

3 Kwa nini lugha wanazonena ni za kufanana? yaani neno 'ndo' lazima liwemo ni kweli neno hilo lina maana halisi katika lugha za wanadamu au ndo kupoteza wakati?

Amini usiamini wengine wanajilazimisha kunena kwa lugha wengine tayari wana mapepo yanayowaongoza kuongea lugha za ajabu zisizo na maana kwa wanadamu na kibaya zaidi ni kuwa Wachungaji wamewaaminisha waumini wao kuwa wanenapo lugha hizo means tayari wana Roho Mtakatifu ndiyo maana usishangae mwizi, mchawi na hata mwongo wananena kwa lugha, Je, Roho Mtakatifu akaa kuchafu?


Nadhani nimejibu hoja nzima uliyoweka hapa

Mungu akubariki .
 
Uko sahihi mia mia,Hakuna kunena kwa lugha siku hizi,huwezi kuropoka 'bashokro bashantu bujaeterii vaaavaaa,gruut zraaa'halafu unadai unanena kwa lugha wakati kimsingi hakuna kinachoeleweka hayo huwa maigizo,Roho mtakatifu aliwashukia wanafunzi wale na kuwapa nguvu ya kunena kwa lugha ili ujumbe ufike kwa watu kutoka mataifa mbalimbali waliokusanyika Yerusalemu kwa wakati ule,kimsingi roho humwezesha mtu kunena kwa lugha ili injili iwafikie watu fulani wa lugha ile,na sio kupiga kelele zisizokuwa na mpangilio wala maana isiyoeleweka.
 
Nimejibu hapo kwenye uzi wa kwanza. Matendo 1:8 inasema nanyi mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roh.Mt nanyi mtakuwa mashahidi wangu toka uyahudi samaria hata mwisho wa Nchi. Nguvu inayozungumzwa hapa ni nguvu ya kuhutubu,kuponya,kutoa pepo na kuyaishi maisha matakatifu.Kumtambua mtu mwenye Roho mt.Kunaambatana na mifano hiyo. Kunena kwa lugha ni ishara tu ya Roh.Kumwingia mtu.Hivyo hii haina faida yeyote kama hakuna mabadiliko mengine.Ndivyo Paulo alivyofafanua.
 
Back
Top Bottom