Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,028
- 59,657
Sipo hapa kulaumu,
Ila kuna jambo najaribu kuliweka mezani...
Kuna kundi kubwa sana la vijana nadhani ndio nguvu kazi ya taifa, hawa vijana toka kipindi cha JK walikuwa wanalalamika ajira hakuna, uchaguzi ukapita salama* na sasa hivi ni awamu nuingine mpya.
Ni wazi hili kundi limesahaulika kabisa, na mkuu wetu sidhani kama ana mpango wowote wa kuwasaidia hawa vijana kwa nionavyo mimi.
Kinachotokea ni mchaka mchaka kama headmaster anavyoongoza shule ya sekondary. Kwanza huwezi kunyanyua ulimi wako kujibishana na headmaster never.
Sasa nini mstakabali wa hili kundi?
Wakalime? Haiwezekani wote kwenda kulima. Hapa kinachotakiwa ni kila mtu binafsi kwa uwezo wake akomae tu kivyake vyake.
Sasa swali linakuja mambo yakizidi kuwa mabaya nini kitatokea kwa sababu ni wazi mwenye shibe tayari ameshamsahau mwenye njaa, kutokana na mtizamo wake anajiona yupo sahihi sana ila watu wanaumia huku akiwa hana hata interest ya kutaka kujua hali halisi.
Kigezo chake anasema watu walikuwa wapigaji.
Kasahau yeye alikuwa ndani ya huo mfumo kuliko sisi vijana ambao hata hatujui kitu, kwanza tulikuwa hata hatujui kuwa kuna wafanyakazi hewa, yeye alikuwa kwenye system kwa muda mrefu sana aliona na anajua.
Hao wapigaji na watu wa madili anaodhani wanaumia sasa hivi wala hata hawaumii.
Wanaoteseka ni kundi lingine kabisa ambalo hata halijawahi kuwa kwenye system, wale wapigaji anaowasema yeye sasa hivi wamejitune na wanaendelea na maisha yao ya kawaida sana na hakuna hata mmoja anayeisoma namba.
Hapa ninachokiona ni wrong approach to wrong person.
Kila kitu kipo wazi, graduate yupo kitaa anakula vumbi unamuambia alizoea upigaji, kuna uhalisia hapo?
Je nini hatima ya hili kundi kubwa sana hapa Tanzania ?
Mtizamo wa Saint Ivuga sio mtizamo wa JF