kama alivyoandika mmoja wa waachangiaji, tatizo kubwa ni uwiano wa mahitaji ya mwanamke na mwanamme na vilevile tabia, mazoea au ujuzi wa mwenzio, kila mtu anamahitaji yake, pengine yeye anavyokufanyia anahisi anakuaonyesha mapenzi ya hali ya juu, na inawezekana anakupenda sana lakini kwako wewe huoni kama anamapenzi kwako,
kubwa ni kumsoma mwenzio, chukua muda kuongea naye na kumueleza ungependa akufanyie nini, akuambie maneno gani nk,
inawezekana aibadilike au aikufanyie immeadiately lakini atakuwa anafahamu nini unahitaji na with time atajifunza!! na atakufikisha upatakapo, fahamu kwamba mmetoka katika mazingira tofauti na pengine wote mlikuwa na wapenzi wa aina tofauti wakiwa na needs tofauti sasa kubadili si kazi ndogo, play your part, fanya kila uwezalo to be good wife, mueleze nini unapenda na unahitaji kwa mapenzi na upole (wanaume hawapendi kulazimishwa) mpe muda afanye mabadiliko, usichoke!!
tafadhali usijaribu kusema ngoja nimjaribu fulani namuona ana mapenzi labda atanifanyia nitakavyo utajidanganya, wanaume wanavyoonekana sio walivyo, na ndio maana marafiki au wanaokuzunguka wanakuona unapendwa!!
pia fahamu kuwa sie akina mama huwa ni ngumu ku-appreciate hiyo ni weekness yetu, mara nyingi tunaona hatupendwi au hatuthaminiwi, ondoa hiyo dhana na utaona tofauti, appereciate kwa kidogo anachokufanyia ili umpe moyo atende mazuri zaaidi!!