Kunaubaya kumuonyesha mpenzi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kunaubaya kumuonyesha mpenzi...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by 007/Mrs.bond, May 8, 2009.

 1. 007/Mrs.bond

  007/Mrs.bond Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wako kua unampenda? Je ni kitu gani watu kama hawa hupoteza au hupata faida wanapolificha penzi kwa mweza wake? Maana nimejaribu kulichambua hili swala sipati jibu...nasikia tuu kwa watu na marafiki wa karibu na Mr. kuwa Duh, mmeo anakupenda sana. Sasa inakuwaje kwangu hanionyeshi! naombeni ushauri katika hili.
   
 2. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hebu fafanua, kipimo chako cha mapenzi ni nini?
   
 3. 007/Mrs.bond

  007/Mrs.bond Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mimi kuwa mwanamme ananipenda
  1. awe muwazi
  2. awe na mda nami
  3. anionyeshe upende mbele za watu, yani awe karibu nami nitokapo nae out
  4. aniachie mambo ya jikoni niyasimamie mimi kama mwanamke
  5. asiwe mbahili wa pesa
  6. aniheshimu n.k

  Hayo ni baadhi tuu katika kipimo changu.
   
 4. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duh, requirements nyingi sana ndio maana hawezi kutimiza. wanaosema anakupenda perhaps wana-base on two or at most three criteria.
  1. kuna level za kuwa muwazi la sivyo utaharibu
  2. muda inategemeana na lifestyle, kazi n.k
  3. watu wengine wana mapenzi ya ndani sio lazima waonyeshe outwardly [hii pia mie yanishinda]
  4. jikoni inategemeana, siku hizi watu wanaongelea gender equality, ama perhaps ndio mapenzi yenyewe hayo, anakusaidia!
  5. ubahili inategemeana na planning, na utofauti wa mitizamo kitu muhimu kwako chaweza kuwa sio muhimu kwake, inabidi mkae chini muongee vizuri
  6. hii sawa, sidhani mtu atakupenda halafu asikuheshimu
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  the tehe tehe.....nyie si mnataka haki zenu ati muwe sawa na wanaume....gangamara na wewe uache kupiga mizinga kwa hubby wako.....
   
 6. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #6
  May 11, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  navyofahamu mimi haikatazwi kumuonyesha unayempenda pendo lako kwake, atakua anakuonyesha ila si kwa kiwango unachotaka wewe, ila dada Mrs 007 unapaswa ufahamu ndani ya mapenzi ili yaendelee kuwepo lazima uwe na mikakati ya upendo wako, ebu chukulia kama ni chakula mfano unachokipenda sana, ukaenda sehemu ukakikuta kisha ukapewa kama sahani tatu ukazimaliza,nadhani hamu ya hicho chakula itakwisha lakini kama utapewa nusu sahani lazima hamu itabaki,na ukumbuke huyu anayekupa nusu sio kwamba hana, ana ghala nzima la hicho chakula, na kwenye mapenzi mambo yanafanywa kwa mipaka,lazima kuwe na mipaka ili pendo liendelee,sasa ukitoa yote ndugu yangu kesho si utakua huna jipya?
   
 7. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa maana hiyo Kifaru huyu Mrs 007 amefanya yeye kosa kuonyesha penzi lake kwa huyo jamaa! au unamaanisha na yeye apunguze penzi? Kweli JF kuna mambo, makubwa haya sijawahi kuyasikia ati. Ehe hebu nihabarishe mengi nisoyajua nami!
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...nakweli!, akiyatoa yote na bado haaminiwi ndio utakuta mtu kaacha ujumbe "nimeona bora nife uamini nakupenda na siwezi kuishi bila wewe!" :(
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  kwi kwi kwi! unaujua mchezo wa DRAFT au SOLO? huu mchezo ukiwa ndani unacheza kete huzioni lakini wa pembeni hata wewe ukitoka nje ukakaa pembeni na kuangalia unakuwa unaziona sana kete na kusema dah umeiacha kete ile ilikuwa nzuri sana kuicheza hii ni sawa na mapenzi shemeji wa nje ndo wanao jua na kunotice mambo.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  dada Penny JF ni zaidi ya uijuavyo!
   
 11. 007/Mrs.bond

  007/Mrs.bond Member

  #11
  May 12, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante ndugu kwa kunifungua macho, kwa kweli nilikuwa naumia sana nikisikia haya mambo kutoka kwa marafiki zake...kumbe dawa na mimi nipunguze speed from 180 to 90! Je, sasa hapa natakiwa nifanye nini hasa!
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwenye kupunguza speed kuna mawili,...utakugongwa kwa nyuma, au kuna ataye ku- overtake!

  ...ni bora u- maintain speed at a safe distance. Rekebisha tu side mirrors zako, pamoja na rear na front morrors huku ukijihadhari na mabonde, milima, matope na utelezi ambavyo vyote vinaweza kukusababishia ajali na kilema cha kudumu. :)

  'Akili kumkichwe!'
   
 13. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #13
  May 13, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Kama ambavyo ukijiremba au ukivaa nguo nzuri huwezi kujitazama mwenyewe na kujikubalia kuwa umependeza hadi umwulize au usike toka kwa mtu mwingine akikwambia umependeza (ambayo kina mama wanaipenda saaan) ndivyo na kwenye kupendwa kunaweza kuwa. Unataka aonyeshe vipi mbele za watu ikiwa watu haohao ndiyo wanaokwambia kuwa mumeo anakupenda!.

  Kwa wale waliosoma Sociology kuna mchoro fulaqni ambao mukiwa kundi halafu mkaambiwa kuuangalia kwa makini na kusema mnachokiona, kunakuwa ni taswira zaidi ya moja ambayo kila mmoja anaziona (sura ya msichana mrembo, bibi kizee, kikombe, n.k.). Yawezekana mapenzi ukawa unayaona lakini kwa taswira tofauti tofauti, hali ambayo inaweza kuwa inasababishwa na mazingira tofauti. Wakati mwingine hisia za umiliki wa mpenzi wako zinaweza kukufanya ukawa huyaoni mapenzi yale kwa kina kinachostahili badala yake ukaona kama haki ambayo unastahili kuipata kama mwanandoa
   
 14. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kabla sijakujibu, ningependa uelewe ya kwamba mapenzi ni uhusiano wa watu wawili. Kama unatafuta mtu atakayetimiza uliyoyataja, inabidi nawe uwe na list ya mambo ambayo utahakikisha naye pia atapata

  Kwa mfano

  1. utakuwa muwazi
  2. utampa muda kamili wa kukaa na wanaumme wenzake bila kupiga simu au kununa atakaporudi
  3. Useme unachotaka bila ya kutumia mapenzi au kitendo cha mapenzi kupata
  4. Ujue hali yake ya maisha na uweze kuishi ndani ya budget hiyo
  5. Uwe muelewa na usijiachie i.e baada ya kuolewa usishinde kutwa na khanga mbili (ujitahidi kuleta "sex appeal"
   
 15. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #15
  May 13, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  penyy, hapana simaanishi kumuonyesha mwenzio upendo ni vibaya wala mrs 007,hajafanya vibaya ila tatizo alilokua nalo ni kwamba anaona sasa yeye anatoa sana kwenye mahusiano na hapohapo hakuna anacho receive,au ana receive kidogo than anachotoa, ebu angalia huu mfano:mtu anatakiwa akifanya kitu kwenye uhusiano basi kuwe na uwiano na mwingine anachofanya,ebu angalia mpigie simu mwenzio mara moja au mbili kisha msubiri yeye naye akupigie,hata hata kama ni mara moja lakini siku nyingine unamfanya akupigie mara mbili wewe unampigia mara moja,hutoweza ona kama hupendwi ila ukiwa unapiga kwa sana ndo utaona hupendwi,utahisi labda unajipendekeza, inakua ngumu kuweka mipaka ila ni nguzo moja tu inayoweza kukusaidia,jisemee moyoni ,kwani akiondoka ndo mwisho wa maisha yangu,ukiona unaogopa uje uko utumwani ndugu yangu, halafu kuna kingine lazima tukifahamu mwanaume na mwanamke ni vitu viwili viliyokua katika mila tofauti,na wote wana tofauti ya kuona jinsi wanapendwa,yaani vitu anavyoangalia mwanaume kama anapendwa ni tofauti na anavyoangalia mwanamke,lakini cha ajabu, vitu hivyo vinategemeana,mfano: mwanamke ukim-care anaona unampenda wakati mwanaume anataka appreciation,sasa ona mwanaume anayetoka safari kambebea mkewe zawadi,mwanamke lazima amu-appreciate jamaa,na jamaa anafeel lovely kwa ajili amekua appreciated,
  hapo unakua ulimwengu wa lovely kwa kwenda mbele,ila penny sikushauri upunguze pendo lako kwa mzee ila cha muhimu uwe unajaribu kuweka vitu katika uwiano,
   
 16. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,028
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  .

  Soul sidhani wake zetu (na wanawake kwa ujumla) hili litawaingia. Kwa watu jinsi KE: kila mwanaume anapokuwa nje ya nyumba basi yupo nyumba ya kulala wageni anazini. Iwapo watakusikia na kuufanyia kazi basi nyumba nyingi zitakuwa salama na upendo utatamalaki
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  May 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Naam, hata kandanda ukiwa nje ni rahisi kusema lile goli la wazi kabisa ukiingia ndani unapata kigugumizi cha miguu. Mrs Bond nina swali, je wewe unamuonyesha mumeo jinsi unavyompenda kwa penzi lako lote?
   
 18. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #18
  May 14, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,028
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  We Missed Our Lady
  The ladies of the World they look like,
  But differ in structure.

  And why she?
  All have got beauty faces,
  Decorated with pink and whitish powder;
  As beautiful rose flowers decorating a beautiful garden.

  But why she?
  Educated girls as she;
  Stays indoor like a curtain inside the house,
  Fighting for freedom, freedom of love.

  But why she?
  She was not free, free for love.
  Kept on weeping day by day.
  Where is this person, so called freedom?

  But why she?
  Love knocking at her door;
  She was not aware.

  But why she?
  Its arrival caused havoc to her;
  Harassment, harassment, harassment by men,
  Where are we now and what do they want?
  Love? Is it possible?
  Oooh! We have missed our lady!
   
 19. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #19
  May 14, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Safi sana kwa kunipa jibu zuri sana, sasa nadhani kama mmlalamikaji alivyosema hapo inawezekana yeye hapewi hiyo care atawezaje ku appreciate hapo sasa.
   
 20. Grader

  Grader JF-Expert Member

  #20
  May 14, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 446
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kabla ya kumlaumu mmeo hebu hayo yote uliyoyasema unayafanya kwake kwani ikumbukwe ya kuwa mapenzi hayana fomula kama mahesabu ya darasani,ikumbukwe ya kuwa wanaume wengi katika utafiti mdogom nilioufany unaonyesha ya kuwa wanaume wanaotoka au wanaokuwa na nyumba ndogo sababu yao kubwa ni kukosa wanachokusudia kukipata baada ya kuoa kabla ya hapo alikuwa anapata bila ya kukosa kipindi cha uchumba.
   
Loading...