Kunani kati ya NSSF na Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support

KIBONGOMKUTI

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
1,425
606
Wanabodi kwa mujibu wa Sheria za Tanzania kila Mwajiriwa mwenye Mkataba wa muda au wa kudumu huwa anakatwa mafao ya hifadhi ya jamii.

(a) Kampuni ya ulinzi ya Knight Support inawakata Mafao ya hifadhi ya Jamii Wafanyakazi wake lakini inaelekea kuna mchezo mchafu kati ya Watumishi wa NSSF ambao wana shughulika mafao ya Wafanyakazi wa Knight Support kutokuwa makini pia kutoa ushirikiano.

(b) NSSF wana Fao la Matibabu ambalo Wanachama wa muda mrefu wanastahili kupata kama sehemu ya kupunguza makali ya maisha pindi Mwanachama Mchangiaji anapopatwa na maradhi au Wanakaya wake. Fao hili halitekelezeki kwa Wanachama Wachangiaji wa Knight Support ambao tumekuwa tunakatwa mishahara yetu zaidi ya miaka 10 iliyopita lakini kila siku majibu wa Wafanyakazi wa NSSF ni mepesi eti Mwajiri wenu HALETI michango kana kwamba hawana wajibu wa kufuatilia japo tumekuwa tunawapa hadi ushahidi wa Salary Slip iliyokatwa michango husika.

(c) Mamlaka ya Nidhamu au Utawala ya NSSF ifanye uchunguzi mwepesi itabaini kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na ukiukwaji mkubwa wa Haki za Wafanyakazi Wachangiaji wa Knight Support kwa kushirikiana na wabadhirifu wachache waliopo NSSF.

(d) Kwa kuzingatia kuwa Knight Support ni Kampuni inayofanya Biashara endapo itaamua kuondoka nchini au kuacha Biashara kuna uwezekano mkubwa zaidi ya asilimia 100% Wafanyakazi Wachangiaji wa NSSF kulia kilio cha majonzi makubwa kutokana na uzembe, wizi, ufisadi na kutowajibika kwa Wafanyakazi wa NSSF wanaosimamia mafao ya Watumishi wa Kampuni ya Knight Support.

Hili nalo ni jipu linaenda kinyume na Sheria za nchi pia hata maagizo ya Mheshimiwa Raisi John Pombe Magufuli.
 
Mkuu

Mkuu kwa ushauri mdogo tu fanya hivi. Kama wewe ni miongoni mwa wahanga wa kadhia hiyo. Waandikie barua ofisi za NSSF zinazohusika na makampuni kama hilo ulilolitaja (Nadhani address kwa Manager). Copy peleka kwa SSRA halafu fuatilia mwenyewe. Usisubiri mambo yaharibike make kama ulivyosema kampuni inafanya biashara, siku ikifunga biashara ukakuta account yako haina kitu unaweza kuzimia au kupoteza maisha. Kwa hali ilivyosasa mbona ukiwaandikia Copy kwa Mkurugenzi mkuu wa NSSF na SSRA watakujibu na watalifanyia kazi suala lako.
 
Asante kwa ushauri nitazingatia tayari kuna baadhi Statement zetu za NSSF haziendani na makato yetu lakini hatupewi uhsirikiano
 
Mkuu, pole sana, hapo NSSF kuna compliance officer ambaye anavuta Knight support, inawezekana hawapeleki michango halafu akija mtu wa kukagua wanamvutia mpunga, cha msingi fanya kama mdau alivyokuelekeza hapo juu.

Hii iliyokea katika kampuni yetu tuletewa charge ya 16mil Kwa kuchelewesha michango (kama penalty) japokuwa tulikuwa tumeshapeleka michango yote (tulikuwa tunapeleka kila baada ya miezi 3) kulingana na namna tunavyolipwa na client wetu) jamaa alikuwa anasumbua anataka tumpe 3 mil iyo ishu ife nikamkomalia na kuandia nssf barua kwa nini nilikuwa nachelewesha michango na namna mtu wao anavyotaka nimpoze...mpaka leo hii wamekoma na sisi tumekoma kutopeleka michango kwa mda
 
Nilikuwa mwajiriwa wa kampuni tajwa kwa muda wa miaka mitatu na nilikuwa nashughulikia issue ya nssf, kwa kifupi hakuna nafasi ngumu kwa knight support kama kudeal na issue ya nssf ngoja niishie hapa
 
Asante kwa ushauri nitazingatia tayari kuna baadhi Statement zetu za NSSF haziendani na makato yetu lakini hatupewi uhsirikiano
Mkuu huwa unamuona Mh. Rais Magufuli anapokuwa anaongea kuhusu nchi hii kuibiwa??
Mkuu wa nchi anasema tumeibiwa sana. Na ni kweli tumeibiwa sana. Kuanzia maofisini kwetu. Huko nyuma (miaka 10-15 iliyopita) Taasisi za serikali zilikuwa zinapokea pesa moja kwa moja kutoka Hazina (pesa za mishahara). Kilichokuwa kinafanyika ni baadhi ya taasisi kutowalipa wafanyakazi kwa wakati kwa kisingizio kuwa pesa bado hazijaja kwenye taasisi zao. Kumbe huku kwa mlango wa nyuma tayari pesa zilishakuja, wameshirikiana na watu wa Hazina, Wizara na benk (wasio waadilifu) kufungua account fixed na kila mwezi hizo pesa wanaziingiza kwenye hiyo account yao kwa kipindi cha muda wa hiyo fixed account (eg mwezi mmoja) wakishapata interest yao wanazitoa ndo wanalipa mishahara. Kama utakumbuka ofisi nyingi za serikali watu walikuwa wanalalamika kucheleweshewa mishahara. Mshahara wa mwezi huu kwa mfano unalipwa katikati ya mwezi wa sita
 
NSSF wakishiriakiana na Idara ya kazi hawana muda wowote wa kufuatilia wanaokataa kuwasilisha michango ya wajiriwa wao, kila siku utawaona kwenye ofisi za waajiri wanaofuata sheria. Ukiwapa taarifa kuna kampuni mwanachama wao haiwasilishi michango wanakuambia nenda kashtaki kwenye tawi lako la chama cha wafanyakazi. Kama mwajiri ni member wao kinachowanyima kumfuatilia nini?
 
Hawa NSSF ni shida sana haswa kwenye swala la kufuatilia michango iliyocheleweshwa na mwajili/Waajili.
Nakumbuka mwaka juzi wakati wa maonyesho ya biashara pale Sabasaba tulikutana na legal officer Mmoja wa NSSF na kumjulisha matatizo ambayo kipindi hicho yalikuwa yanatukabili kama wafanyakazi na wahanga wa kucheleweshewa malipo yetu ya nssf.
Sisi tulitaka atupe ushauri tu nini tufanye, lakini hata ushauri wa nini cha kufanya hakuwa nao zaidi ya kutueleza kuwa yeye analetewa tu malalamiko internally na kuyafanyia kazi kwa kuwapelewa mahakamani waajili ambayo wamechelewa kupeleka michango ya wafanya kazi wao.
Kwa sababu tulikuwa wengi kiasi, tuliamua kuachana nao hao jamaa na kutafuta mwanasheria wetu. Tuliamua kumshitaki mwajili wetu kama mshitakiwa wa kwanza na benki ambayo alikuwa anatumia kupitishia pesa zake. Kesi tulishida na hivyo mahakama ikaamua mwajili kupitia benki ilipe haki zetu zote ikiwa pamoja na NSSF. Kwahiyo malimbikizo yote ya NSSF yalilipwa moja kwa moja na benki kwa amri ya Mahakama. Ila ilikuwa mlolongo kidogo, kwani hata NSSF tulitaka awe mshitakiwa namba tatu ila Mtalamu wetu wa sheria akasema itachukua muda sana ku deal nao jamaa kwahiyo akatushauri tuendele na mwajili. NSSF Shidaa kwa kweli.
Ushauri wangu kwa mleta mada, kama mupo wengi mnaweza mpeleka mahakamani mwajili wenu, na kama upo peke yako waweza enda SSRA wanaweza kusaidia japokuwa sina hakika kama itakuwa kwa haraka sana.

Hapo KST upande wa accounts ni shida saana.
 
Nashukuru saana kwa michango yenu na uzoefu wenu katika harakati za kudai mafao ya NSSF. Najiuliza maswali kadhaa
(1) NSSF inaendeshwa kwa michango yetu Waajiriwa kwa lugha ya Kiustaarabu sisi ndio Waajiri wao inakuwaje Mwajiriwa hataki kumuhudumua Mwajiri na hakuna mifumo ya Kitaasisi ya kushughulika na issues kama hizi hadi twenda SSRA?

(2) Mwajiri anapo chelewesha michango kuna adhabu ukipenda sema Penalty inakuwaje hakuna adhabu kwa Mtumishi wa NSSF asietekeleza wajibu wake?

USHAURI
NSSF ni Ofisi ya umma ni busara au lazima kuweka mfumo rafiki wa jinsi ya kushughulikia malalamiko au kero za Wateja. Mfumo wa mgawanyo wa Madaraka ya Kiutendaji/Maamuzi uwekwe wazi kwenye kila Ofisi. Pia iwe ni wajibu wa Afisa husika kumfahamisha Mteja Haki zake kama hakuridhika na uamuzi/ushauri wake ili tuweze kufikia mamlaka za juu zaidi.
 
Back
Top Bottom