Kunani kampuni ya Vodacom?mbona haigusiki?

Mjasiriamali1

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
891
237
Nilikuwa najiuliza kunani kampuni ya Vodacom? Inakuwaje serikali inawaogopa kuwachukulia hatua? Kuna mkono wa nani huko? Kwanini mamlaka husika zimefyata mkia? kuwachukulia hatua? Je serikali inamuogopa nani? Kule? Pamoja na malalamiko ya uwizi wa waziwazi kutumia vocha na bundle lakini serikali imekaa kimya? Leo wamekuja na staili mpya, ukiweka vocha kwa ajili ya bundle la internet ukisubscribe, hola! hakuna kitu, unaletewa salio lako halitoshi. Tayari wamekwangua shilingi 20, inakulazimu tena ununue vocha ingine uongezee, unaweka data off, unsubscribe siku nzima hakuna kitu, haikubali, unabadilisha bundle la kawaida la cheka lile lenye mb 1, inakubali. Nikanunua vocha kwa Mara ingine safari hiii kabla sijaweka vocha nikawapigia kwanza, kuuliza kulikoni Leo Kuna nini kwenye system yenu ka dada kana nyodo kaniambia wewe uliweka data on! ndo mana salio liliisha kumwambia nilizima hakataki kusikiza kabisa, kanoongea kwa kiburi tena hakakupi nafasi ya kujieleza, kanauliza labla kamaa unatatizo jingine nikamwambia hili hujalisolve unataka lingine, kakata simu, nikapiga tena kupokea wakawa wameshajipanga kupokea tuu ananiambia subiri nikupeleke kwa mtu wa data, walijuaje? Maana ni mteja mpya? Kila anapopiga customer care? kumweleza ananiambia inawezekana ni tatizo la system eti jaribu kuzima simu kuwasha na u switch data off, nishafanya hivyo, anasema jaribu sasa itakubali, nikamwambia vip kuhusu vocha nilizopoteza? Eti ananiambia pole Sana jaribu tena Kama nilivyokushauri, wakati wa kwanza kanijibu kwa kiburi. nikamwambia Jana nimesubscribe data za internet hata sijatumia mkanitumia eti data zangu zimeisha? Nilipopiga mkaniambia sorry ni matatizo ya system! UPUUZI MTUPU,Hapo vip Leo pia mnaniambia eti ni tatizo la system. HAWA JAMAA WANATENGENEZA SCENE YA KULAZIMISHA MTU KUNUNUA VOCHA KWA KUKULETEA MESSAGE ZA UONGO, AU KUKWANGUA DATA ZAKO, NA SI MAKOSA YA MTANDAO, KWA MAKUSUDI KABISA, NA HILI SWALA TCCRA WANALIJUA NA SERIKALI WANALIJUA NA WAMEKAA KIMYA, KWA KUWA SISI WANANCHI HATUNA SEHEMU ZINGINE ZA KUPIGA KELELE! TUNAPIGIA HUMUHUMU. NA MODS, AND INVISIBLE USIJEBADILISHIA THREAD YANGU HII! WACHA IENDE KAMA ILIVYO. MESSAGE SENT.
 
Vodacom ni kama 'small independent nation'
Magufuli atarusha kichura chura watumishi wa serikali tu
huko kwa Vodacom inajulikana konyagi wanalipa kodi kubwa kuliko vodacom
lakini hakuna wa kubadili hali hiyo
 
Vodacom ni kama 'small independent nation'
Magufuli atarusha kichura chura watumishi wa serikali tu
huko kwa Vodacom inajulikana konyagi wanalipa kodi kubwa kuliko vodacom
lakini hakuna wa kubadili hali hiyo
nashukuru kwa kufaham kuwa nikinunua zile bapa najenga nchi kwa kiasi kikubwa kuliko navyonunua vocha
 
Back
Top Bottom