Siku mmoja nikiwa Dar maisha yamekuwa magumu sana coz biashara za madili zilikuwa zimekatika, ikapigwa simu kwa jirani. Wakati huo hakukuwa na simu za mkonini. Aliyepiga simu alikuwa ananiulizia kwa kuwa sikuepo aliipokea ndugu yangu na aliyepiga akamuulza aniulize kama ningependa kusoma.
Hakika sikuamini nilipoambiwa na huyo aliyepokea hyo simu haraka haraka tukaenda pale high way barabara ya mandela kwa wenyeji wa Dar kwenye zile simu za TTCL za kadi, nadhani mnazijua.
Tukampigia huyo mtu simu akasema niende Mwanza nilikuwa natamani kusoma sana tena sana, kwa bahati mbaya baba yangu mzazi hakuwa anajali kuhusu elimu na umaskini nao ulikiwa unachangia ukijumlisha na pombe basi sikuwa na tumaini la kusoma kabisa, ukizingatia wakati huo sekondari zilikuwa chache sana.
Nilifunga safari hadi Mwanza ambapo mama alikuwa akiishi baada ya kuachana na baba yangu kwa miaka kama 20, basi nilipofika nilimkuta mama na mzee mmoja mzee huyo ni wa kingoni jina nalihifadhi, huyo mzee alikuwa mwanajeshi, nikaa kama wiki nzima hakuna anaesema chochote kuhusu kusoma, baadae nzee akasema nimekuita ili nikusomeshe, nilizani ni msamalia mwema ila siku moja mama akaniambia mzee huyu ndie baba yako.
Nilikasilika sana coz nilikuwa namjua baba yangu sasa kwanini nitambulishwe baba mwingine ila mama alinipoza kwa akasema wewe kubali akusomeshe tu hayo mengine utajua mbele kwa mbele, nikamuulza mama ila kwanini yeye aseme mimi ni mwanae, mama akasema wakati wa mimba yangu baba aliikataa na akawa anamtuhumu kuwa ni huyu mwanajeshi ndie alienpa mimba, hivyo huyu mwanajeshi aliamini yeye ndie aliyenipa mimba, ndio maana anataka akusomeshe kwa kweli sikuwa na hiana nilikubali akanisomesha, kwa hiyo bila mama kuchepuka pengine shule ningeisikia redioni.