Kuna utofauti gani kati ya nyumbu wanaohama kutoka Serengeti kwenda Masai mara Kenya?

Nazareti

JF-Expert Member
Apr 1, 2016
413
443
Kila mwaka nyumbu huwa na safari ya kuhama aidha toka mbuga ya Serengeti ya Tanzania na kwenda Maasai Mara mbuga ya wanyama ya Kenya au kutoka Maasai na kuja Serengeti.

Hivyo basi katika purukushani hiyo hawa wanyama hutapatwa na sitofahamu hasa pale wanapojikuta upande wa pili wa mto huku maji yamefurika hadi kingo za mto haziwezi tena kuyazuia.

Basi hapo ndo utajua akili za nyumbu zilivyo maana wao bila hata kutafakari kitakachowapata ndani ya mto huhitaji nyumbu mmoja gaidi atakayejirusha kwaza na baadaye kundi zima la nyumbu huanza kumiminika misiri ya asili ambayo haikatiki hadi iishe yote.

Hapo sasa nyumbu huaza kujirusha ovyo ovyo bila hata kuwaangalia kwanza wenzao waliotangulia nini kimewapata humo mtoni, wala hawawezi hata kubadilisha njia nyingine salama tofauti na pale wakwanza amejotolea muhanga.

Hapo sasa ndo sherehe ya mamba hufikia kilele maana takribani asilimia 60 ya nyumbu hugeuka mizoga baada ya kukanyagana na kuuana wao kwa wao katika heka heka za kujirusha. Ni asilimia 40 tu ndiyo huvuka salama lakini kwa shiida na huku wengi wakiwa wamejeruhiwa hata hawana tena uwezo wa kuendelea na hiyo safari.

Takribani kwa miaka ya hivi karibuni dunia nzima imeshuhudia wimbi kubwa la wenzetu waarabu kuhamia nchi za magharibi safari ambayo kimantiki ni vigumu kuitofautosha na ya nyumbu wa serengeti.

Binadamu wenzetu hawa wanasafiri
safari ambayo wengi wao huishia kuwa maiti ndani ya bahari ya mediterrania jambo ambalo linatuachia huzuni kubwa lakini pia maswali ya kujiuliza. Kimsingi nchi nyingi zote za kiarabu huongozwa na shariah ambayo hutokana ni Imani ya kiislam ambayo ndiyo dini yenye wafuasi wengi katika za zinazotumia kiarabu na zile zenye waumini wengi waislam.

Kuifuata shariah ya Allah na kuiishi ndiyo wito mkuu kwa muislam yeyote kwakuwa kwa imani yao shariah hiyo ndiyo muongozo sahihi mwanadamu anapaswa kufuata. Sasa je ni kwamba watu hawa wemechoka kuishi chini ya hii shariah na sasa wanaona ni bora kuishi chini ya mfumo na utaratibu wa Mungu wa Israel mfumo unaotumiwa na nchi za magharibi na zile zenye Wakristo wengi?

Au wamekandamizwa mno na watawala wao kinyume na shariah ya Allah na sasa wanatafuta kwenda kule ambapo watakuwa huru na dhruma hii?

Chakusikitisha ni kwamba watu hao wanajua yote yanayowapata wenzao humo baharini na wala hakuna mwenye uhakika wa kuvuka salama. Boti zenyewe zinazotumika hazina kiwango cha kuyakabili maji mazito ya bahari, tena boti ya kubeba watu hamsini wanapanda watu mia mbili mara wafikapo katikati ya bahari chombo hicho huzama na asilimia 80 ya wasafiri wadogo kwa wakubwa hupoteza maisha yao na kwetu hubaki na masikitiko na huzuni lakini pia maswali yasiyokuwa na majibu sahihi.

Kama nyumbu vile, je ni kwanini watu hawa pamoja na kuona wenzao wanaishia bahari lakini wao

kwanza tu ndiyo wanazidi kupanga msululu na kumiminika ndani ya bahari? je huu ndiyo utafutaji wa maisha bora au ndiyo ujasiri wa kuigwa? kama waliungana kuwaondoa watawala dictator wao kwanini tena hawawezi kuungana wakaandamana ili kuwafanya watawala wao wapya kuacha kuwanyanyasa? au hayo ni mapenzi ya Allah kwao? au ni nini basi? Isis na magadi wengine ndiyo chanzo? au je imani yao ndiyo tatizo kwamba wanaenda Ulaya ili wapate nafasi ya kusikiliza Injili kwakuwa huko nchini mwao wana wa Injili ni sadaka kwa njia ya visu? tusemeje sasa? ni nani basi atakaye weza kuwasaidia hawa binadamu wenzetu? je twawezaje kuwatofaurisha na nyumbu wa serengeti?

Ukichunguza kwa undani utakuja gundua kuwa kwa misingi ya imani ya dini watu wa magharibi na watu wa dini nyingine ni makafiri kwa imani ya kiislam, mara nyingi watu hao huambulia visu shingoni pindi wajaribupo kuingia kwenye nchi za kiarabu. Lakini hao hao ndiyo wamekuwa waokozi wa hawa watu na kuwaonyesha huruma ya juu kabisa kinyume na wanavyofanyiwa pindi wawapo kwenye nchi za kiarabu. Hakuna mwarabu wala taasisi yeyote ya kiislam inayojishughulisha na uokozi baharini ila watu wa magharibi ambao ni makafri.

Nimetafakari sana maana kila ukifunguliwa vyombo vya habari utasikia leo wahamijai elfu kadhaa wamezama na kupoteza maisha baharini. Hebu Great thinkers tujaribu kuwaza na kutafakari juu ya
hili maana wao pia ni binadamu wenzetu na hawapaswi kabisa kupatwa na yale yanayowapata.
 
Huwa najiulizahuo uhamiaji ni shida au ndio njia za kujitafutia maslahi zaidi kutoka na siasa kandamizi za wafalme wa huko Uarabuni sababu haiji akilini watu wavuke mabonde namilima kwenda Ulaya wakati kunanchi nyingi huko Uarabuni ambazo zina neema kubwa ,nchi kama Saudi Arabia,Lebanon,Kuwait,UAE ,Israel.
 
Waje na Afrika,maana kuna fursa nyingi za kiuchumi na Dunia sasa ni kijiji.
 
Nchi za Ulaya hazina mpango na Mungu wa Israel(Yakobo).
Wana mambo yao tu ndo maana wanaruhusu ushoga.
 
Back
Top Bottom