Kuna uhusiano kati ya uduni wa maisha na kuipigia kura CCM?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,930
2,909
Nimetathimini mwenendo wa siasa zetu hapa nchini nikabaini kuwa maeneo mengi ambayo wakazi wake wana maisha duni sana huichagua CCM kwa kishndo kuliko maeneo yenye nafuu kubwa ya maisha.

Ikumbukwe kuwa mikoa kama Dodoma, Ruvuma, Rukwa, Katavi, Tabora ni miongoni mwa mikoa ambayo wakazi wake hu-struggle sana na maisha huku wakiwa na huduma duni sana kulinganisha na maeneo mengne, wakati huohuo CCM inajivunia kuwa hayo maeneo ndiyo mtaji wake kisiasa.

Je, kuna muunganiko kati ya uduni wa maisha ya wananchi na ushabiki wa CCM!?
 
Watu wana njaa, wanadanganyika na sahani za pilau na kofia na khanga. .

Watu hawana elimu. Bado wanachagua viongozi wakiangalia kabila /dini. Hawaelewi kuwa wao ndo walipa kodi na huduma za kijamii ni haki zao na si msaada wa kiongozi.
 
Ni kuwa kama mtu ana njaa ukimpa ahadi ya shule bora au barabara na ukimpa ahadi ya sahani ya pilau unadhani atachagua kipi? Ni wazi shule au barabara hataviona vya maana zaidi ya pilau aponye njaa yake.
Ahadi za ccm ni misosi
 
Wabunge wa UKAWA wasije kusoma hii thread wakajidanganyana kwamba majimbo yao hayana umasikini. Wakiendelea kususa na kutoka nje ya ukumbi mwaka 2020 watapigwa chini, na hao CCM ambao wanaongoza kwa kuwa na majimbo masikini watayachukua tena hayo majimbo. Kuna yule mmoja alikwenda China kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kununua vitanda na vifaa vya hospitali, yule hawezi kusoma hii thread kwanini ameamua kwa vitendo kushughulika na umasikini wa wapiga kura wake.

Kukosoa, kudharau kile kinachofanywa na serikali wakati mtu amekaa ndani ya nyumba yake ni kitu kimoja, kutembea huko mikoani na kuona hali halisi ni kitu kingine.
 
Kuna dada maisha yake duni sana alishangilia sana siku magu kashinda akiniambia hapa kazi tu! Sasa nikimwambia hapa kazi tu ananinunia maisha duni anaishi chumaba kimoja watoto watatu hata shule za bure hawasomo kazi kubwa anauza genge ambalo saa hizi kalifunga nyumba aliyopanga haina umeme, mweny nyumba anataka weka umeme kodi ikipanda sijui kama atabaki?
 
Umasikini huleta woga
fear of unknown...
huu woga hufanya uogope any change..

unakuwa comfortable na known condition hata kama ni mateso....
Ni kweli mkuu..nchi ilikuwa inaishi na majipu katika kila kona ya mwiliwake...Sasa tumepata jasiri, shujaa ambaye yupo tayari kufanya mabadiriko kwa kuondoa majipu yaliyotesa hii nchi kwa miaka mingi..
 
nimetathimini mwenendo wa siasa zetu hapa nchini nikabaini kua maeneo mengi ambayo wakazi wake wana maisha duni sana huichagua ccm kwa kishndo kuliko maeneo yenye nafuu kubwa ya maisha ikumbukwe kua mikoa kama dodoma, ruvuma,rukwa,katavi,tabora ni miongoni mwa mikoa ambayo wakazi wake hustrugle sana na maisha huku wakiwa na huduma duni sana kulinganisha na maeneo mengne wakati huohuo ccm inajivunia kua hayo maeneo ndiyo mtaji wake kisiasa je kuna muunganiko kati ya uduni wa maisha ya wananchi na ushabiki wa ccm!?
Umetaja mikoa mitano ambayo unasema wana maisha duni ndiyo maana wameipigia kura CCM kwa faida ya JF tutajie mikoa yenye maisha mazuri waliyoipigia kura Chadema.
 
Umetaja mikoa mitano ambayo unasema wana maisha duni ndiyo maana wameipigia kura CCM kwa faida ya JF tutajie mikoa yenye maisha mazuri waliyoipigia kura Chadema.
dar,tanga,arusha,kilimanjaro,mwanza(kabla ya nkapa kwenda kutibua mambo),kagera(nkapa alitaka kuyatibua matokeo ya bukoba manispaa tulicho mfanya hatosahau)
 
dar,tanga,arusha,kilimanjaro,mwanza(kabla ya nkapa kwenda kutibua mambo),kagera(nkapa alitaka kuyatibua matokeo ya bukoba manispaa tulicho mfanya hatosahau)
Umeelewa swali lakini au umekurupuka kujibu mambo ya manispaa sijui nkapa.

Jibu swali mikoa gani ina maisha mazuri wameipigia kura Chadema?
 
Wabunge wa UKAWA wasije kusoma hii thread wakajidanganyana kwamba majimbo yao hayana umasikini. Wakiendelea kususa na kutoka nje ya ukumbi mwaka 2020 watapigwa chini, na hao CCM ambao wanaongoza kwa kuwa na majimbo masikini watayachukua tena hayo majimbo. Kuna yule mmoja alikwenda China kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kununua vitanda na vifaa vya hospitali, yule hawezi kusoma hii thread kwanini ameamua kwa vitendo kushughulika na umasikini wa wapiga kura wake.

Kukosoa, kudharau kile kinachofanywa na serikali wakati mtu amekaa ndani ya nyumba yake ni kitu kimoja, kutembea huko mikoani na kuona hali halisi ni kitu kingine.
we hujielewiiiii,..uko maswi nini/katavi
hii mada ya wadsm
 
Kuna dada maisha yake duni sana alishangilia sana siku magu kashinda akiniambia hapa kazi tu! Sasa nikimwambia hapa kazi tu ananinunia maisha duni anaishi chumaba kimoja watoto watatu hata shule za bure hawasomo kazi kubwa anauza genge ambalo saa hizi kalifunga nyumba aliyopanga haina umeme, mweny nyumba anataka weka umeme kodi ikipanda sijui kama atabaki?
wacha wayaoneeee
malipo hapahapa dunianiiiiiiiiiiiii
ccm inawenyewe
 
Ni kweli mkuu..nchi ilikuwa inaishi na majipu katika kila kona ya mwiliwake...Sasa tumepata jasiri, shujaa ambaye yupo tayari kufanya mabadiriko kwa kuondoa majipu yaliyotesa hii nchi kwa miaka mingi..
Mtumbua majipu gizaniiiii au sio????
hawz kusucced kwa wengine kuwaacha akina ridh mokko,khalfan vasco,
 
Back
Top Bottom