Kuna Uharibifu Daraja la Ruvu, Safari za Treni zasitishwa, Treni za bara kuishi Morogoro..

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE

KUSIMAMISHWA HUDUMA YA TRENI ZA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO MEI 18, 2017

Uongozi Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusimamishwa huduma ya treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017 hadi itakapotangazwa tena.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na Ruvu junction uliosababishwa na mvua kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya mkoa wa Pwani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kusitisha huduma kwa muda treni ya abiria ya deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam leo saa 2 asubuhi imefutwa na abiria wametakliwa wafike stesheni ili warejeshewe fedha zao za nauli.

Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari umeelekea eneo la tukio ili kufanya tathmini na kupanga mikakati ya haraka kukarabati miundo mbinu husika likiwemo daraja la Ruvu.

Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia ya reli kati ya Dar es Salaam na Morogoro itakapofunguliwa tena.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

KampunI ya Reli Tanzania(TRL),

Mei 18, 2017

DAR ES SALAAM

=======

Daraja la Ruvu reli ya kati limekatika. Hakuna treni yoyote kutoka Dar au kuja Dar itakayopita. Mungu tunusuru
532b9c53-29e6-4382-abdd-5f91d3bf324e.jpg
5870846c-9da6-45c6-89c0-d5799fd71728.jpg
24dc7aae-34dd-496f-bf24-68554e337010.jpg
 
Kwani hii siyo Standard Gauge Railway (SGR) itayopita treni ya mwendo kasi..??
Tumshukur Mola hakukuwa na treni ikipita muda huo.
Ingekuwa treni inapita muda huo , ile ajali ya Dodoma ingekuwa cha mtoto.
 
Aisee hii ni hatari, bora halijaleta maafa, lingeleta maafa hela za rambirambi ndizo zingetumika kulijenga, sasa tunataka hela za kulijenga zitoke hazina
Hilo daraja sidhan km litajengwa leo sbb serikali inategemea rambi rambi. Na rambi rambi hakuna, sijui watatoa wap fedha? Ajali ingetokea hapo wala rambi rambi wangefurahi sana, wangepata hela ya kujenga daraja na kulisha familia zao
 
Tushukuru mungu kuna watu hapo wameokolewa kutoka kwenye dhambi ya kula pesa ya Rambi rambi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
kusafiri kwa reli ya kati usalama wake ni 30% ubora wa miundo mbinu 70% huruma ya Mungu tu, maana nahis reli yote imeoza. mbona tazara wao majanga kama haya hawanaga!?
 
Hii reli ilishajichokea kitambo.. Tunasubiri maafa yatokee tupate cha kuzungumza
 
Hali hii imepelekea kukatika kwa mawasiliano kwa pande zote mbili, kutokea Morogoro na Dar Es Salaam..
8d72904a90ceb351c3ba79792a18bccf.jpg
7d1e3c9ff62875dfd9e8f9174c01de5f.jpg
 
Hii inaonyesha jinsi watanzania tunavyolindwa na mungu nasikia hata lile daraja la mto wami halifanyiwagi service lakini roho zinazopitishwa na mola ni nyingi.tumshukuru mungu kila saa.
 
Back
Top Bottom