Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,666
- 729,779
Dunia ya sasa fashion ni recycling ili kuokoa malighafi na kupunguza uchafu. Kwamba ukinunua chupa ya maji ukishayanywa ile chupa huitupi tu ijaze majalala, inapata matumizi mengine na mwisho inakuja kuzaliwa upya tena na kuwa chupa safi kabisa.
Kuna vingi vya kufanyia recycling na kwakweli vimeokoa rasilimali nyingi huku ajira mpya pia zikizalishwa...recycling ni jambo jema sana kwa muktadha huu.
Siasa zina mambo ya ajabu sana lakini moja kuliko yote ni kuwa na kiwango cha juu cha unafiki na uwezo wa kuhubiri usichokiamini huku ukiamini usichokihubiri.
Siasa za kiafrika zina shida kubwa sana kwenye hili, Siasa za visasi na kukomoana, kwamba kuchafuana ni jambo la kawaida kama tusipoenda sawa! Nitasimama kwa nafasi yangu na kuonyesha umma jinsi usivyokuwa na uwezo wa kufanya majukumu yako! Lakini ukinifuata privately tukayajenga kesho narudi kuwa mshkaji wako na unanifikiria tena kwenye ulaji.
Inakuwaje jana tujinasibu na damu changa huku tukiwaseta wazee kuwa ni goigoi na wapenda mlungula lakini kesho tuwatafutie tena ulaji?
Tunahitaji Katiba mpya kama tuna nia ya kusonga mbele...binadamu hafanyiwi recycling