Ni wilaya inayopatikana katika mkoa wa lindi ambayo kwa sasa inaongozwa na mbunge mh. Mathias Chikawe,wazir wa katiba na sheria katika serikaali yetu tukufu ya awamu ya nne iliyoko chini ya Prof.Kikwete.Kinachonisikitisha ni kwamba hali ya kiuchumi katika wilaya hii ni ngumu mno,hakuna masoko yenye tija ya bidhaa za ufuta,mbaazi na korosho.Miundo mbinu ni aibu kabisa na suala la umeme ni kama hadith iliyokosa mwendelezo. Cha ajabu sasa wananchi hawashtuki,Chikawe hashituki,na hata vyama vya upinzani havijashituka.Ni nani katuloga viumbe sisi? kuna nini Nachingwea?