Kuna nchi za kuingia bure ila hii hapana, Sudani kusini yatoa ruksa kwa raia wa Tanzania hakuna ulazima wa visa

Kuna nchi za kuingia bure ila hii hapana, Sudani kusini yatoa ruksa kwa raia wa Tanzania hakuna ulazima wa visa

Fbn

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
15,760
Reaction score
37,366
Hivi mwenye akili unaweza kwenda huko

1784641102865.png

--------------------

Sudan Kusini imetangaza utaratibu mpya wa viza ambazo zinawapa raia wa nchi mbili tu za Afrika, Tanzania na Misri, fursa ya kuingia nchini humo bila kuhitaji viza.

Chini ya sera hii iliyoboreshwa, raia wa Tanzania na Misri wanaweza kusafiri kwenda Sudan Kusini bila kulazimika kuomba viza mapema wala kulipia gharama zozote zinazohusiana na viza.

Miongozo hiyo mipya pia inaeleza kwa kina mahitaji ya kuingia nchini humo kwa wasafiri kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika na kwingineko duniani, ikifafanua utaifa wa wale wanaostahili kuingia bila viza pamoja na ada zinazopaswa kulipwa na wale wanaohitaji viza.

Raia wa nchi zingine za Afrika, ikiwemo Ghana na Nigeria, hawana sifa ya kuingia bila viza na hivyo wanatakiwa kupata viza na kulipia ada zilizowekwa kabla ya kufanya safari.

Wasafiri wanashauriwa kukagua mahitaji ya hivi karibuni ya kuingia nchini humo, orodha ya nchi zinazostahili, pamoja na gharama za viza kupitia chanzo rasmi cha serikali ya Sudan Kusini kabla ya kupanga safari zao.
 
Zitaje kwa faida ya wengi.
Nchi imepata uhuru 2012 kama sikosei tena Africa unadhani ukiwa mjanja hutoboi kama Tanzangiza tu ina mifupo corrupt ya kuwa tajiri sembuse huko nchi rais mzee hadi hana kumbukumbu anajikojolea hadharani.
 
Ilikuwaje Tanzania na Misri ndo zikapewa hiyo fursa? wataalam wa diplomasia mtujuze.
 
Back
Top Bottom