Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,335
- 13,293
Kwa muda mrefu sasa toka enzi za Mkapa serikali imekuwa ikikosa fedha za kutosha kukamilisha bajeti ya mwaka! Hii ni kwa sababu serikali imekuwa ikishindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yatokanayo na kodi na vyanzo vingine vya mapato zikiwemo fedha za wahisani kutokutolewa kwa wakati.
Ili kuondokana na adha hii ya kukosa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo na kuendesha serikali, inabidi mkakati wa kuondokana cash budget uandaliwe ili kuwe na akiba ya kutosha ambayo itatumika kwa maendeleo na kuendesha serikali. Kwamba fedha zikusanywe mwaka huu wa fedha ili zitumike mwaka ufuatao wa fedha!
Vinginevyo wizara zitaendelea kupata fedha chini ya makadirio kila mwaka!