WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 935
Kama msomi tu hana uthubutu au hajitambui au ni muoga kudai haki zake, je kwa HOUSE GIRL au HOUSE BOY itakuaje?
Staff ya Chuo cha Sebastian Kulowa Memorial University na wanafunzi wake wote wapo kwenye COMA yani sintofahamu, wanafunzi hawajui lini wanafanya mitihani na hawajui lini watafunga chuo, huku ma-lecture hawajui lini watalipwa sababu iliyopo nyuma ya pazia kuwa hawana vigezo.
Ilikuaje utawala wa chuo au maaskofu waliajiri watu wasio na vigezo? Ni aibu kwa taasisi zinazohusika na kuandaa taifa la kesho linakuwa na uzembe kama huu.
Wizara ya elimu, sayansi na teknolojia kama taasisi husika inapaswa kuingilia kati katika swala hili, na inapaswa tambua kuwa wanafunzi wengi walio chuoni hawana fedha za kujikimu (wategemea BOOM) na muda wa kukaa chuoni unazidi kuongezeka kwa uzembe wa utawala wa chuo.
Wizara ya ajira, nayo inapaswa kuwajibika kama wizara inayosimamia maslahi ya watumishi binafsi na seikalini, ma-lecture waalipwe fedha zao tena na fidia juu.
Wanafunzi wa SEKOMU wakiandamana kesho na kesho kutwa wanatumiwa defender za FFU bila hata kuwasikiliza kwa nini walikuwa au wameandamana, kundi la watu haliwezi kuandamana bila sababu maana sio kundi la vichaa au wenda wa zimu lazima serikali ikubali kusikiliza sauti za wananchi wake bila kujali itkadi ya aina yoyote.
Chuoni kuna mgomo wa chini chini, staff ipo kwenye mgomo baridi. Mgomo huo unaathiri wanafunzi bila hatia yoyote.
MTANZANIA AWE AMESOMA AU HAJASOMA BADO ATAENDELEA KUWA MTUMWA.
HII INATHIBITISHWA NA STAFF YA SEKOMU.
HII INATHIBITISHWA NA STAFF YA SEKOMU.