Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 10,664
- 22,844
Unapokuwa unatafuta ushauri wa kimahusiano kwaajiri ya kujijenga na kutibu changamoto za kimahusiano ni vizuri kufahamu wapi kwa kwenda.
Wengi wetu hutafuta washauri ambao huja katika sura mbalimbali kwa mfano, Wazazi, walezi, wachungaji, wataalamu wa saikolojia, relationship coaches, dada na kaka zetu, marafiki zetu wa karibu sana, wadogo zetu, watu tunaofanania jinsia na umri au rika etc. Mtu yoyote unaemfuata kwaajiri ya ushauri huyo tunamwita ni counselor.
Watu hawa bila kujali wanatokea katika category ipi huwa wanaangukia katika magroup mawili ya wajenzi au wabomoaji wa mahusiano.
Unaweza kupewa ushauri mzuri wa kukutoa katika changamoto ya mahusiano unayopitia kwa sasa ila baadae ile changamoto ukaja kutambua kuwa haikuwa ni changamoto bali ni hatua ya kimaisha ambayo ulitakiwa kuihimili na kuivuka ili ukue kiakili na kuweza kuhimili maisha kwa urahisi.
Ni wanaume wangapi waliambiwa au kushauriwa kuwaacha wake zao kwasababu hawapati watoto kisha wakaenda kutafuta mke mpya kutatua changamoto ya uzazi lakini wakaja kusikia yule mke wa zamani amepata mtu mwingine na kapata watoto vizuri bila shida ila yeye amebambikiwa watoto na mke mpya.
Au haujawahi kuona kisa cha mwanamke aliyeishi na mwanaume kwa miaka 15 ya maisha ya kuunga unga kisha akajipa majibu yakuwa huyu mwanaume hatokuja fanikiwa maishani akaamua kuvunja uhusiano kwa kiburi na dharau halafu miaka 5ntu tokea amuache mwanaume huyo anakuja kusikia habari kuwa huyo bwana maisha yamemkalia vema amekuwa tajiri kupita maelezo.
Nyuma ya maamuzi,aidha mazuri au mabaya huwa hakukosekani washauri. Ni vema kujiuliza aina ya washauri wanaokuzunguka wewe wanatokea kundi gani.
Kama ni marriage/relationship Counselor then hapa utapata watu wa kukupa namna ya kuelewa unachokipitia na kinakupeleka wapi kupata nini lakini watakupa tiba ya kiakili ya kupata njia za kudeal na pressure ya changamoto huku ukijipanga upya kujijenga.
Kwa upande wa pili kama washauri wako ni marriage/relationship cancellers then jua hapa utapewa kila sababu ya kukimbia na kuipekua changamoto ambayo pengine unapokwenda utakutana na nyingine kubwa kushinda hii. Wao watakufundisha namna ya kukwepa wajibu wako kwa mwingine na kukushauri ujitazame na kujiweka wewe kwanza kabla ya mwingine hata kama unaweza kumsaidia.
Kwa kifupi, kuwa makini unapokea na kuomba ushauri kwa nani.