Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.
Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?
Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.
Nawasilisha.