Kuna Majogoo wa Jirani wanawika Saa 6 hii ya usiku je ni Majogoo kweli au ndiyo wale Ndugu zetu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,535
Tangia nizaliwe ' hakyanani ' sijawahi kusikia ' Jogoo ' akiwika / wakiwika mida hii ya Saa Sita ( 6 ) za usiku kama huu ila nashangaa muda huu naandika huu ' uzi ' huko nje nyumba ya Jirani ' Majogoo ' yameanza ' kuwika ' tena kwa fujo na yanapokezana.

Je hawa ni ' Majogoo ' kweli au labda wale Ndugu zetu ( Wachawi / Wanga ) ndiyo wanaitana sasa ili kufanya ' parade ' yao ya kuanza kutuchosha kwa ' kutulimisha ' na ' kutubebesha ' mizigo mizito usiku kucha huu?

Naombeni msaada wenu tafadhali kwani kwa ' kuwika ' Kwao huku hawa ' Majogoo ' tayari nimeshaingiwa na hofu hasa ukizingatia siku mbili hizi kila nikiamka najikuta nimechoka mno halafu miguu ina vumbi tupu utadhani nilikuwa nafyeka uwanja wa Simba SC kule Bunju.

Nawasilisha.
 
GENTAMYCINE. Hao wametoka Shamba wakiona Umeme hudhani kumekucha

Na mbona sasa wakiwika wanaelekezea Shingo na Sauti zao upande wa dirisha langu Mkuu? Nimewakosea nini? au labda wanadhani na Mimi nipo pengine katika list ile ya Makinikia hivyo wanataka ' kuninyoosha ' kwa ' kuniadhibu ' mapema? Hii sijapata kuona katika maisha yangu yaani ' Majogoo ' yanawika mapema hivi Saa Sita ( 6 ) hii kweli! Ninavyojua wengi muda wao wa kuwika huanzia Saa 9 usiku au Saa 10 alfajiri ila hii ya Saa 6 hii ndiyo naishuhudia rasmi leo tokea nizaliwe. Na hata huko Vijijini huwa naenda kutembelea na wanafuga sana hawa Kwiyo Kwiyo / Kuku ila huwa ' hawawiki ' Saa 6 kama hawa.

Halafu hata Biblia yangu nayo nimesahau nilipoiweka kwani ni muda mrefu umepita tokea niishike achilia mbali kuifungua tu na kusoma ' maandiko '. Leo nitakiona cha moto ' wajameni '.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom