Kuna majipu sekta ya Afya mkoa wa Mbeya

Utapiamlo

New Member
Mar 17, 2016
1
0
Toka kale kadada kachaguliwe kuwa kaganga kafawidhi, kaliundiwa mitandao mingi sana ili katolewe, kwa sababu hakakutoka miongoni mwa kundi la watu toka njia panda ya Chalinze.

Kenyewe kanacheka nao, kakidhani ni marafiki. Maskini wee. Wenzako walitaka upigwe chini nafasi yako apewe fizishani wa hapo hapo kwako au toka hospitali ya rufaa Mbeya.

Walishindwa tu. Wengine wanadai ofisi za juu za tiba na meno kimkoa zilihusika, na mfanyakazi mmoja kwa RSO na mkuu wa maadili mkoa.

Bahati mbaya kwao bidada hajui lolote, akawa anachapa kazi hadi wakaamua ku retreat.

Kako clean mwee, kamepelekewa auditors kwa kukashtukiza kutokana na majungu lakini hola. Kanachapa kazi sana, hata tulipokachunguza tuliona mapato yameongezeka. Kapo kazini hadi jumapili, utadhani hakana familia.

Ila pia mulika xray, kuna mtu anaitwa Haule, anajifanya mashine ya Xray ni yake. Ati yeye anajiita uwt. Sijui kama aliacha siku hizi kununua xray film zake mwenyewe.

Anaamua muda wa kufunga na kufungua ofisi ya xray. Waiteni watu waliopigwa pesa na huyu jamaa. Hata wenzake wa idara moja hawaivi.

Kuna dokta anaitwa Dani. Yeye kutwa nzima anahamisha wagonjwa toka hospitali ya mkoa na baadhi toka hospitali ya rufaa Mbeya, kuwapeleka kuwatibu private zake kwa KS. Anajiita daktari bingwa wa mifupa!!! Atamzidi hata doctor Benny kwa umashuhuri wa kukata miguu.

Huyo mganga mkuu wa mkoa naye ni jipu. Kazi wafanye wao sifa apokee yeye. Kila siku anataka madaraka, mara atake ubunge, mara ukatibu mkuu, mara atake ukurugenzi wa rufaa.

Nasikia alijaribu kumshawishi yule waziri wanayetoka naye Tanga ampe ukurugenzi wa hospitali ya rufaa Mbeya wakati hata nafasi aliyoshika sasa haistahili.

Usisahau na pesa za ukimwi za wamarekani zilivyoliwa. Hapo toka hospitali ya rufaa Mbeya, hadi kwa msimamizi wa ukimwi mkoa na mawilayani.

Nasikia kuna mtu Rungwe kapata ubunge kwa pesa hizi za ukimwi.

Mulika Makala Mulika!!!
 
We jamaa kwa majungu haujambo...au ulikosa mgao nini?Hata kada ya afya mna majungu hivi?Nakubaliana sasa na utafiti wa kwamba sisi wa Tz hatuna furaha,maana uliyeleta hii nyuzi sidhani kama una furaha.......any way kwa kumsaidia zaidi Makala mtumie hata barua pepe na ushahidi wa tuhuma zako.
 
sasa mkuu mbona ni rufaa tu , kwani uchunguzi wenu haukufika hospitali ya wilaya ya kyela ? hebu funguka vizuri mbona mganga mkuu wa mkoa Dr Mhina anasifika kwa uchapakazi na kujituma ?
 
Weka details, maneno yenyewe tu haitoshi. Unapomzungumzia mtu hafai, au fisadi mwagika details zako humu,tofauti na hapo yatakuwa ni majungu
 
Mkuu Utapiamlo umefanya vyema kutoa taarifa kama hii; kama ina ukweli yamkini mamlaka husika zitakuwa na habari kwa sehemu. Maeneo mengi hutokea ugomvi kwa sababu ya issue za pesa, hivyo serikali ichunguze hili hapo.

Majungu na wizi upo maeneo mengi ya kazi nchini ikiwamo sekta ya afya. Lakini hudhani ku post kwako hii thread kutaharibu amani zaidi kati ya hao wahusika? Maana kuna kila dalili kwamba kuna mtu alitaka kunyolewa na watu anaodhani rafiki zake wa karibu.

Lakini serikali ichunguze hii miradi ya afya inayofadhiliwa na nchi za kigeni, hasahasa HIV na TB. Huko watu wanapiga sana pesa. Hata miradi ya kutoa magovi tu umetajirisha baadhi ya watu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom