Mkuu mimi naamini mahusiano kama hayo yapo. Ila vilevile ni imani yangu kuwa aina hii ya mahusiano kwa kiasi kikubwa inaendana na tamaduni za jamii husika na kiwango cha maendeleo..yote ya kiuchumi na kifikra.
Ukichukulia jamii zetu za kiafrika na kitanzania kwa uhalisia utaona kuwa tupo kwenye zama ambazo mwanamke anaamini ana kitu cha kuuza na mwanamme anaamini kuna kitu anatakiwa kununua kwa mwanamke..kwa mahusiano kama haya unafiki lazima utawale. Mwanamme anaona ana haki ya kununua hicho kitu mahali pengine iwapo akijisikia maadam pesa ni yake na mwanamke anaamini anayo haki ya kumuuzia mnunuzi zaidi ya mmoja maadamu mzigo ni wake.
kwa wenzetu kama ulaya hali hii kidogo ipo tofauti maana wenzetu wamepiga hatua zaidi katika kufikiria kwao kiasi mwanamke anaona akiingia katika mahusiano kwa ajili ya kupata kitu fulani basi thamani yake anakuwa ameishusha na kuwa sawa na bei ya kitu hicho anachokitarajia kupata.
nikirudi kwetu ni kuwa kuna wanawake wachache wanaoamini katika mahusiano ya kweli, yasiyo na unafiki..na kwa upande mwingine kuna wanaume ambao wanaamini katika hilo. Tatizo ni JE, HUYU MWANAMKE MWENYE KUAMINI KATIKA TRUE LOVE ATAFANIKIWA KUKUTANA NA MWANAMME ANAYEAMINI KATIKA TRUE LOVE? WATATAMBUANA NA KUANZA MAHUSIANO? Thats the million dollar question.